Josh Michael
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,523
- 87
Wapo watu wengi sana katika Zanzibar labda ngoja waje nao na wengine wakina Shamuhuna, na Khatibu naye anafaa tuzanzibar hakuna mwingine(KWA MTIZAMO WA HARAKA HARAKA)....
au uniambie ungependa awe nani?
ni kweli Karume Ally anayo haki ya kugombea lakini mi nadhani kwa busara tu asigombee ili isionekane kama urais wa Zenj ni ufalme wa hiyo familia, jee sisi wa familia za wakulima kule Ileje tutapata hata udiwani kweli???/
Vipi Dr Hussein Mwinyi?
Asante, hii ni haki yake kikatiba na lazima iheshimiwe.Kwa hakika Ali Abeid Amani Karume, bila ya kujali jina lake, anayo haki ya msingi ya kikatiba, kugombea nafasi yoyote katika nchi yake ya Tanzania kama alivyo na haki ya kupiga kura na kumchagua kiongozi yeyote anayemtaka. Ni unyanyashaji na ubaguzi wa hali ya juu sana kumnyima haki yake hiyo.
Kama wananchi wataona kuwa hafai kwa sababu moja au nyingine basi wasimpe kura zao wakati wa kura za maoni au za uchaguzi rasmi wenyewe. Mnyonge mnyongeni na haki yake mpeni.
.Tatu kwa wanaomjua wanasema ni kiongozi fulani hapendi kusikiliza la mtu kama marehemu baba yake (yaani hashauriki) hili litamwia ngumu kwani utawala wa ubabe kama baba yake ushakufa zamani watamwangusha hata miezi sita kufika kama akichaguliwa.
Mwinyi mtu fresh ila tatizo unajua Zanzibar kuna siasa za majimbo Salmin ni mtu wa Kusini, Amani ni mtu wa kaskazini na Mwinyi ni mtu wa kaskazini sasa hilo litakuwa kikwazo kwake Zanzibar maana akina Gharib Bilal na kundi lake wanaona ni haki yao na zamu yao kushika hatamu patakuwa patamu hapo.
Mie navyoona watoe mtu kutoka Pemba CCM kwasababu itawasaidia kupata support Pemba na pia kuondoa makundi zanzibar.
Wazanzibari wanaamini Mwinyi+Karume sio wanzanzibari, Salmini ndo anaonekana kama ndio mzanzibari halisi Mwinyi wanadai ni mtu wa kisarawe, karume malawi, huyu karume Ali hawamfahamu saana kwani hajakaa sana huko ila kuna kundi linaamini jamaa anamsimamo na anaweza wanasua na jinamizi la Muungano ila kashfa ya ubakaji na mauwaji bado ipo kwenye kumbukumbu za walio wengi na ukumbuke hawa wanzanibar wanauhusiano wa karibu mno tena ule wa damu so usishangae ali akakosa nafasi ya kuridhi kiti cha ufalme kutokana na hiyo kadhia aliyotenda miaka hiyo