Ali Kiba aanzisha lebo yake, Abby Skills na Jokate wapata shavu

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Imekuwa ni kama fashion sasa kwa wasanii wa Bongo Fleva kwa kila mmoja kutaka kuwa na lebo yake. Ukiachilia mbali wale ambao walikwishatangulia kwenye mambo hayo na lebo zao zikafanya poa.



King Kiba ameitobolea siri Perfect255 kuwa yuko katika maandalizi ya kurudi rasmi katika suala hilo la kusimamia wasanii (Kuanzisha Lebo) na tayari kuna wasanii ambao amekwishafanya nao mazungumzo na watakuwepo chini ya
lebo hiyo.

“Me record lebo ninayo muda mrefu, lakini sikuifanya matangazo, lakini kuna wasanii ambao nilikuwa nawamiliki nikapumzika, sasa hivi narudi tena najipanga upya kama unavyomuona Abby Skills anafanya kazi vizuri na bado ataendelea kufanya kazi zingine, Abdu Kiba pia ametoa ngoma hivi karibuni lakini haijafanya vizuri lakini ngoma ijayo itakuwa ni ya mimi na yeye. Pia kuna msanii mwingine ambaye watu hawajawahi kumsikia, pia kuna wakina Jokate, kina Dalila na wengine kibao tu ambao wapo chini ya Lebo
yangu.”
 
Afanye kitu tofauti na tofauti hionekane sisi wadau tuta muunga mkono
 
mambo mengine buana! sasa kama alikuwa hatangazi nini kimemfanya atangaze?
Mdogo ake alishaulizwa kwanini hawi karibu na kaka yake akasema yeye anataka kutoka yeye kama yeye bila kuegemea kwa kaka yake


Sasa hayo ya leo tunaite mashikoro mageni
 
Nachokikubali kwa domo alikuwa akiwaangalia wakina Kiba na Wema nahisi akiwemo Jokate akijiuliza ee Mwenyezi Mungu ni lini nitakuwa kama hawa watu leo hii cheki yupo juu zaidi yao.

Funzo ni tupige kazi kwa bidii tukimuomba Mungu kwa juhudi zote bila kusahau kuwaheshimu wazazi, Mungu ni mwema , kuhusu ushirikina mimi sishauri
 
Kama wasanii wenyenye ndo hawa
Abdu kiba
Abby skillz
Jokate
Labda waanzishe lebo za shule, kwa muziki wataumbuka....
Ila si nayeye anamilikiwa na label za ROCKSTAR 4000 na SONY AFRICA
Kumilikiwa sio ishu hata davido yupo chini ya sony lakini ana lebo yakea ya OBO, sema changamoto kwa kiba ni hao aina ya wasanii aliowasanisha abdu kiba, jokate na abby skills hawana talent ya music kihivyo na sio watunzi wazuri labda awabadilishe
 
AHAHAHHAHHA
nna lebo ila nilikuwa siitangazi!
sasa ulikuwa nayo ya nini?
af wanamuziki wenyewe ndo kina Abdu na Abby skills (huyu wa leo)
achene ,masikhara bhaaana!
 
anaanzisha lebo ila hapendi kiki...
yeye mwenyewe ameshindwa kuji-manage sembuse hao wasanii wengine[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]...

kiba sio kila kitu cha kuiga jamani!!
vingine viwapite
 
Ni jambo zuri kuwa na Lebo kwa ukubwa alio nao, ila kama kweli anania ya kufanya kazi asiweke lebo kuwafurahisha washkaji zake na madem zake, atafute wasanii wenye vipaji ambao wanaweza kusimama wao kama wao, hao kina Abby Skills na Abdu Kiba walishaprove failure, Blue na wewe mmejaribu kuwabeba sana lakini hawafiki popote. So kuwa siriaz bro, hiyo ni kazi
 
kama ni kweli, hakuna msanii hata mmoja Hapo,, Hawezi Akawa serious
 
Kweli Diamond ndio kioo cha Alikiba...
Yaani Alikiba anachanganyikiwa na Diamond saaana..
Anataka afanane nae kwa kila kitu...hajui kama hivi vitu vinahitaji muda
WCB Inamnyima usingizi saaanaa maskini[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Upo chini lebo, na wewe tena una lebo. Haya yote huwa yanawezemana Tanzania tu.
 
Hivi huyu jojo kwanini hajitambui kwenye mahaba kujitoa akili kutoka na hao bongo fleva zipu wazi ukiachana nao habari zako zooote gazetini sijui amelishwa nini huyu binti
Status yake haiendani na hao bongo fleva ajiheshimu
 
Naanza. Ninanyumba mbagala ila nilikua sijaitangaza
Sababu mm king mswati sipendagi kiki

Nina lebo yangu siku nyingi ila nilikua sijaitangaza tu sababu mm sipendagi kiki
Huyu king mswati ana Matatizo kweli lkichwani
Vingine usiige kaka mwenzie kajipanga kimuziki ajarudishwa kwenye gemu kwa nguvu ya kelele za mashabiki
King mswati atakua amesikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…