Ali Kiba anaingilia ugomvi wa Ommy Dimpoz na Diamond kwa 'quote' hii?

Hapana! Kiba amempongeza diamond hapo.. Maana ameajiri vijana wenzake wengi sana na kwa kweli amewatoa kwenye maisha magumu..

Hongera diamond na hongera kiba kwa kumpongeza kijana mwenzako!

(Subiri waje sasa [emoji23] )
 
Mbona sielewi hapo huu si ujumbe wa MO DEWJ mbona mnapenda kugeuza vitu?
pole kama hujaelewa hapo Kiba alitaka Mond amsaidie Dmpoz kwa kumtafutia collable na features Davido/Iyanya na ndomana katoa hiyo quote kwa sababu Mondi ni msanii mwenye mafanikio hivyo basi asiendekeze starehe bila kuwaangalia waanga wenzake kwa kuwashika mkono Hivyo basi Mondi kwa maono hayo ya Kiba kwamba Dmondi kashindwa kula na kipofu.
 
Daaa kweli kuna watu wachochezi yaaan kisa kapost kiba mbona mo ndio post yake haukuona ameingilia ugomvi wa huo
 
Yaani bado hata sijaelewa we unathibitisha vipi kwamba hiko ulichokiandika ndio Ali kiba amemaanisha ili nikubaliane na hayo mawazo yako.
 
Nilichojifunza ni kua bifu za wasanii zinakuzwa na watu wa pembeni ili maisha yao yaende.Mfano toka mondi na sepetu wawe katika good terms kuna watu wengi sana hawajalipenda hilo maana hawaingizi siku.
 
Mwanaume ukipangishia nyumba lazima upumulie
Sasa dimpoz kapangishia na wale walie filisi bandari. Unategemea mini hapo
 
Pamoja na starehe nyingi anazozifanya Diamond, ila ndiye msanii pekee Tanzania aliyesaidia vijana wengi wasio na kipato kwa kuwainua kiuchumi, kifkra na kimaisha pia. Kupitia WCB, ameweza kuajili vijana zaidi ya thelathini ambao wanajipatia kipato kupitia juhudi za Diamond. Kwa maana hiyo kama ni kupima mafanikio kwa kigezo cha mchango kwa wale wasio na kipato, basi Diamond hana mpinzani katika wasanii wote Tanzania.


Sehemu ya team ya WCB Band
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…