Ali Kiba anaingilia ugomvi wa Ommy Dimpoz na Diamond kwa 'quote' hii?

Ali Kiba anaingilia ugomvi wa Ommy Dimpoz na Diamond kwa 'quote' hii?

Pamoja na starehe nyingi anazozifanya Diamond, ila ndiye msanii pekee Tanzania aliyesaidia vijana wengi wasio na kipato kwa kuwainua kiuchumi, kifkra na kimaisha pia. Kupitia WCB, ameweza kuajili vijana zaidi ya thelathini ambao wanajipatia kipato kupitia juhudi za Diamond. Kwa maana hiyo kama ni kupima mafanikio kwa kigezo cha mchango kwa wale wasio na kipato, basi Diamond hana mpinzani katika wasanii wote Tanzania.

View attachment 439324
Sehemu ya team ya WCB Band
Eeeenh! Hawa wote wanaenda Mayotte?Shikamoo Chibu.
 
Hapo itakua Dewji ndio kaingilia ugomvi...[emoji23][emoji23] ukosefu wa ajira na sarafu mtaani kunafanya akili zetu zinadumaa.
 
Sasa hii ndo mnasema anaingilia ugomvi hapa, hebu acheni uchochezi toka mwanzo Ally na Nasibu wanaugomvi hapo haijalishi kua anaingilia
 
sasa hapo kuna mtu katajwa kwani, wabongo sisi
 
pole kama hujaelewa hapo Kiba alitaka Mond amsaidie Dmpoz kwa kumtafutia collable na features Davido/Iyanya na ndomana katoa hiyo quote kwa sababu Mondi ni msanii mwenye mafanikio hivyo basi asiendekeze starehe bila kuwaangalia waanga wenzake kwa kuwashika mkono Hivyo basi Mondi kwa maono hayo ya Kiba kwamba Dmondi kashindwa kula na kipofu.
Acha kupotosha watu iyo masage ni ya mo akiwahasa watu na kiba kashare iyo masage xx izo tafsiri zako sijui umetoa wapi acha kutafuta kiki kwa vitu vya kijinga
 
hayo maneno ni ya Ali Kiba au Dewji?

Siku nyingine Tumia akili
 
Hapana! Kiba amempongeza diamond hapo.. Maana ameajiri vijana wenzake wengi sana na kwa kweli amewatoa kwenye maisha magumu..

Hongera diamond na hongera kiba kwa kumpongeza kijana mwenzako!

(Subiri waje sasa [emoji23] )

Sijui nimechelewaje kuona hii
[emoji23] [emoji23] [emoji23]

Kwahiyo unataka kusema hiyo quote haimhusu Kiba pia?
Kwani yeye hajatoa ajira kwa vijana wenzake?

Nyie watu bwana!Sishangai thou...kila muwamba ngozi....

Asante kwa pongezi anyway...zimefika [emoji6]
Nanyi hongereni.[emoji122]
 
Mbona sielewi hapo huu si ujumbe wa MO DEWJ mbona mnapenda kugeuza vitu?
Mkuu ndo wabongo tulivyo wavivu kusoma na kufikri mbali tunaendeshwa na matukio.......
 
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi bure kabisa!
 
Huyo wivu wa mafanikio ya mwenzie unamsumbua
Hizi akili sijui mnaziokota wapi .Lini Ali Kiba aliwahi kumzungumzia Diamond hadi useme kuwa anamuonea wivu.Hiyo quote inamhusu vipi Diamond hapo!!Rubbish.
 
Pamoja na starehe nyingi anazozifanya Diamond, ila ndiye msanii pekee Tanzania aliyesaidia vijana wengi wasio na kipato kwa kuwainua kiuchumi, kifkra na kimaisha pia. Kupitia WCB, ameweza kuajili vijana zaidi ya thelathini ambao wanajipatia kipato kupitia juhudi za Diamond. Kwa maana hiyo kama ni kupima mafanikio kwa kigezo cha mchango kwa wale wasio na kipato, basi Diamond hana mpinzani katika wasanii wote Tanzania.

View attachment 439324
Sehemu ya team ya WCB Band

Wengine wapo chini hapo wanapiga picha,,,!'
 
Sio kila kitu kinahusiana na huo ugomvi inawezekana kacomment bila kuhusianisha na ugomvi wao...pia hata yeye Ali kiba ana mafanikio yake kiasi ingawa kazidiwa na Mondi...
 
Back
Top Bottom