Ali Kiba asaini mkataba na Sony Music, South Africa





Mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba kuanzia leo atakua mikononi mwa Sony Music kuanzia leo, kampuni kubwa ya muziki inayofanya kazi na mastaa wa dunia kama Beyonce, John Legend na Chris Brown.

Moja ya kazi za mkataba huo ni kumtengeneza Alikiba kweye kiwango cha juu zaidi kimuziki, kibiashara na kugharamia video zake na anaporekodi audio zake, kila anapotoa muziki mpya unaachiwa kwa nguvu ya usimamizi wa Sony Music kwenye masoko makubwa ya muziki kama Marekani, Ulaya na Africa.

Sio kila msanii wa Afrika ameweza kusaini na Sony Music ambapo nimeambiwa kwenye shughuli hii ya leo kwamba mkataba aliosaini Alikiba unafanana kabisa na ule aliosaini mwimbaji staa wa Nigeria Davido ambapo unavipengele vya kusababisha kolabo kwa urahisi zaidi na mastaa wakubwa wakiwemo wa Marekani.
 
Em ngoja tusubiri hizo album. Tuhifadhi maneno
 
Good for him

Kiba ni wakat WA kupiga kaz, tunategemea hautatuangusha
 
upande wa pili tunawasaidia tshu mkafutie mapufuu[emoji23] [emoji23]
 
Mimi nadhani hii taarifa ina mapungufu au pengine mimi sijaelewa.
Ali Kiba amesign mkataba na Sony Music Africa. Yaani ni Sony Music division ya Africa.
Mmojawapo ya wasanii waliopo kwenye lebo hiyo ni Rose Muhando.
Nakumbuka msanii mwengine Nakaaya aliwahi kusaini na Sony Music Denmark yaani Sony Music division ya Denmark.
Lakini niliwahi kumsikia katika kipindi cha mkasi kama sikosei akisema anajutia kuingia ule mkataba maana ulimuharibia muziki wake.
Nafikiri sio jamba jipya sana kwa wasanii wa Africa.
Wakati mwengine hii mikataba ni mizuri na wakati mwengine ina maumivu yake makubwa.
Hata ukifuatilia nchi zilizoendelea kama USA wasanii wengi wamekuwa wakitoa malalamiko namna mikataba kama hii inavyowanyonya.
Refer: kesi ya Lil Wayne na Cash Money Records,Mase na Bad boy,Buster Rhymes na Cash Money,50 cent na Interscope na mikataba mingine kadhaa.
Unakuta wakati mwengine katika 100% ya mapato ya msanii basi kampuni inachukua 80% . Na msanii anabaki na 20%.
Ninachofahamu Davido amesign mkataba na SONY WORLDWIDE. Yaaani Division ya Marekani ambapo ndio makao makuu ya Sony na mkataba wake nilisikia alipewa advance ya $1000,000 yaani Bilioni 2 na ushehe kwa shilingi za kitanzania. Sijajua upande wa Ali Kiba.
 
Hivi Rose Muhando naye si ana mkataba na Sony?
 
Safiiiiiiiii Kuna jamaa atakuwa anakaribia kupasuka
 
Le mutuz amempongeza Kiba kwa ku team up na Sony,lakini amemuonya kwamba Rose Muhando akiwa chini ya Sony walikutana na hapo hapo Rose akampiga mzinga Le mutuz wa laki mbili- Le mutuz was like what the hell,isnt she supposed to be a Sony baby- kwa shingo upande aka part na laki mbili
 
Yaani hawa jamaa ni majipu... hakuna msanii ambae wamepata kuwa nae Afrika kwa miaka ya karibuni na kisha aka-excel! Lakini kv naona ni kama wanakuja kivingine; I hope wamerekebisha madhaifu yao!
 
chige ebu nitoe tongotongo kdg hiki kifupisho chako huwa kina maana gani "kv" huwa kinanishughulisha kweli nisomapo comments zako.
 
Mkataba wa alikiba haujataja Kiasi cha pesa
Na mara nyingi huwa haitaji issue za mkwanja! Maranyingi ni albums recording, promotion and distribution huku wakikuachia shows zako! So, kama wanakuwezesha kufika mbali, you can benefit alot kupitia show zako kv utakuwa finally well known across your region and all people around the world from that region.
 
uwo ndio mengine kufurahisha genge
 
Watu wengi hawaelewi hata nini maana ya kiba kusaini Sony, wanadhani sasa kiba kawa balozi wa Sony.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…