Ali Kiba asaini mkataba na Sony Music, South Africa

Ali Kiba asaini mkataba na Sony Music, South Africa

4a984d1fb7e345f1a5141e8eafd0ef1e.jpg
3a3252480526c8d63aeb340ded6d768b.jpg




Mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba kuanzia leo atakua mikononi mwa Sony Music kuanzia leo, kampuni kubwa ya muziki inayofanya kazi na mastaa wa dunia kama Beyonce, John Legend na Chris Brown.

Moja ya kazi za mkataba huo ni kumtengeneza Alikiba kweye kiwango cha juu zaidi kimuziki, kibiashara na kugharamia video zake na anaporekodi audio zake, kila anapotoa muziki mpya unaachiwa kwa nguvu ya usimamizi wa Sony Music kwenye masoko makubwa ya muziki kama Marekani, Ulaya na Africa.

Sio kila msanii wa Afrika ameweza kusaini na Sony Music ambapo nimeambiwa kwenye shughuli hii ya leo kwamba mkataba aliosaini Alikiba unafanana kabisa na ule aliosaini mwimbaji staa wa Nigeria Davido ambapo unavipengele vya kusababisha kolabo kwa urahisi zaidi na mastaa wakubwa wakiwemo wa Marekani.
 
upande wa pili tunawasaidia tshu mkafutie mapufuu[emoji23] [emoji23]
 
Mimi nadhani hii taarifa ina mapungufu au pengine mimi sijaelewa.
Ali Kiba amesign mkataba na Sony Music Africa. Yaani ni Sony Music division ya Africa.
Mmojawapo ya wasanii waliopo kwenye lebo hiyo ni Rose Muhando.
Nakumbuka msanii mwengine Nakaaya aliwahi kusaini na Sony Music Denmark yaani Sony Music division ya Denmark.
Lakini niliwahi kumsikia katika kipindi cha mkasi kama sikosei akisema anajutia kuingia ule mkataba maana ulimuharibia muziki wake.
Nafikiri sio jamba jipya sana kwa wasanii wa Africa.
Wakati mwengine hii mikataba ni mizuri na wakati mwengine ina maumivu yake makubwa.
Hata ukifuatilia nchi zilizoendelea kama USA wasanii wengi wamekuwa wakitoa malalamiko namna mikataba kama hii inavyowanyonya.
Refer: kesi ya Lil Wayne na Cash Money Records,Mase na Bad boy,Buster Rhymes na Cash Money,50 cent na Interscope na mikataba mingine kadhaa.
Unakuta wakati mwengine katika 100% ya mapato ya msanii basi kampuni inachukua 80% . Na msanii anabaki na 20%.
Ninachofahamu Davido amesign mkataba na SONY WORLDWIDE. Yaaani Division ya Marekani ambapo ndio makao makuu ya Sony na mkataba wake nilisikia alipewa advance ya $1000,000 yaani Bilioni 2 na ushehe kwa shilingi za kitanzania. Sijajua upande wa Ali Kiba.
 
Hivi Rose Muhando naye si ana mkataba na Sony?
 
Leo Akiwa South Africa Alikiba Amesign Sony Music ,Lebo hii ambayo inawasimamia akina Chris Brown,Davido na John Legend itakuwa na Kazi ya kutangaza video na Audio za Alikiba Kimataifa na Duniani kote

Nitaleta Taarifa kamilii hapa!

=======================

Habari wapenzi wa burudani,

Yule nguli wa Bongo Fleva na staa wa Bongo Fleva, Ali kiba amesaini mkataba leo na kampuni ya Sony Music jijini Johannesburg,South Africa, moja ya vitu vilivyomo kwenye mkataba huu ni kampuni hii kubwa ya muziki duniani kusimamia pia video zake na audio kwa kuzilipia na kuzifikisha kwenye masoko makubwa ya muziki duniani.


View attachment 348941

Ali Kiba ameungana na mastaa wengine duniani waliosign Sony Music kama Davido (Nigeria) , Chris Brown ( Marekani) ,John Legend na wengineo.

Baada ya kusaini mkataba na SonyMUSIC leo, sasa kazi zake zitasimamiwa na SonyMusic duniani kote ambao watasimamia kazi zake kwa kiwango cha kimataifa, hiyo ni moja ya vitu watafanya

View attachment 348942

=======
Tanzanian singer and songwriter Alikiba, Sony Music Entertainment Africa and ‪major african record label ROCKSTAR4000‬ have a groundbreaking announcement to make!

Just a few weeks after Davido signed a major deal with Sony Music, ROCKSTAR4000 is proud to announce that Alikiba will be the second major African artist signing with the prestigious label and will also be the first from East Africa.
Safiiiiiiiii Kuna jamaa atakuwa anakaribia kupasuka
 
Kipaji peke yake hakitoshi bila kuwa na timu inayofahamu tasnia ya muziki! Kiba kipaji anacho lakini hana timu ya maana kwahiyo sio mbaya akiwajaribu Sony!

Nasema kuwajaribu kv Sony Africa wame-prove failure! Labda wabadilike sasa baada ya kufanya some reorganization.

Binafsi nashindwa kuielewa business model yao manake set up yake tu tayari inawaandaa ku-fail. Ukichukua wasanii kutoka Sony Music Entertainment na subsidiaries zake wanaweza kufika 200 na zaidi kutoka sehemu mbalimbali duniani!

Sasa unapokuwa na idadi kubwa ya wasanii namna hii; wasanii kutoka hizi nchi zetu hawawezi kupata privilege waipatayo wasanii wao waliopo kwenye label kubwa kubwa kv Columbia Records au RCA. Kwahiyo mafanikio ya watu kama akina Kiba yatategemea sana na management ya Sony Music South Africa Office na sio Sony yenyewe ya US na ndio hata hawa waliopo; kwa Anglophone anaefanya vizuri ni AKA peke yake! For Davido it's too early to say! D'banj amebaki kulilia collabo tu toka kwa akina Chibu!

But all in all, as I said earlier; kv Kiba hakuwa na timu ya maana basi sio mbaya akiwajaribu! Muhimu ni kutokuwa too optimistic na porojo za kutangaziwa muziki wake dunia mzima!! Hizi ni porojo zisizo na maana yoyote cuz Sony wana wanamuziki kibao toka nchi za Asia, Ulaya, Oceania hadi Middle East... mbona hatuzioni kazi zao huku!!?
Le mutuz amempongeza Kiba kwa ku team up na Sony,lakini amemuonya kwamba Rose Muhando akiwa chini ya Sony walikutana na hapo hapo Rose akampiga mzinga Le mutuz wa laki mbili- Le mutuz was like what the hell,isnt she supposed to be a Sony baby- kwa shingo upande aka part na laki mbili
 
Le mutuz amempongeza Kiba kwa ku team up na Sony,lakini amemuonya kwamba Rose Muhando akiwa chini ya Sony walikutana na hapo hapo Rose akampiga mzinga Le mutuz wa laki mbili- Le mutuz was like what the hell,isnt she supposed to be a Sony baby- kwa shingo upande aka part na laki mbili
Yaani hawa jamaa ni majipu... hakuna msanii ambae wamepata kuwa nae Afrika kwa miaka ya karibuni na kisha aka-excel! Lakini kv naona ni kama wanakuja kivingine; I hope wamerekebisha madhaifu yao!
 
chige ebu nitoe tongotongo kdg hiki kifupisho chako huwa kina maana gani "kv" huwa kinanishughulisha kweli nisomapo comments zako.
 
Mkataba wa alikiba haujataja Kiasi cha pesa
Na mara nyingi huwa haitaji issue za mkwanja! Maranyingi ni albums recording, promotion and distribution huku wakikuachia shows zako! So, kama wanakuwezesha kufika mbali, you can benefit alot kupitia show zako kv utakuwa finally well known across your region and all people around the world from that region.
 
Na mara nyingi huwa haitaji issue za mkwanja! Maranyingi ni albums recording, promotion and distribution huku wakikuachia shows zako! So, kama wanakuwezesha kufika mbali, you can benefit alot kupitia show zako kv utakuwa finally well known across your region and all people around the world from that region.
Watu wengi hawaelewi hata nini maana ya kiba kusaini Sony, wanadhani sasa kiba kawa balozi wa Sony.
 
Back
Top Bottom