Ali Kiba aufyekelea mbali YouTube wimbo wa 'Hela' baada ya kushukiwa na mashabiki wake kutoa wimbo mbovu

Ali Kiba aufyekelea mbali YouTube wimbo wa 'Hela' baada ya kushukiwa na mashabiki wake kutoa wimbo mbovu

labda target yake alijua nyimbo itapendwa ili atambie kwenye fiesta kama alivyofanya mwaka jana na ile seduce me, ila mambo yamemwenda vice versa.
 
kwanza mimi si shabiki wa timu wala mtu. mimi naheshimu na napenda kazi nzuri.
hivi huyu jamaa hanaga watu wa kumshauri. msanii mkubwa kama yeye anatoa nyimbo mbovu mpaka unashangaa, management inaruhusu vipi nyimbo mbovu kama hela itoke eti ndio nyimbo mpya.

ishu sio kutaka ashindane. Maua sama, Aslay wanatoa nyimbo kali wanashindana na nani? kila akifanyacho hakina uelekeo. kaanzisha kinywaji, hata maendeleo yake hakieleweki. promo ya hiyo biashara zero. Mara kasajiliwa na team hata kucheza hatuoni yaani amekuwa kama mtu wa kutapa tapa. Afanyi kitu asilimia mia kikaeleweka. Kiukweli ana asset kubwa sana ya mashabiki waliyenaye bega kwa bega ambayo hata wasanii wengine wanatamani lakini anawaangusha sana. itafika steji watamchoka.

sasa kulikuwa na lebo rockstar4000 leo tena naona kuna kingsmusic sijui.

huyu jamaa ni msanii mzuri ila watu wanaomzunguka hawamtakii mema. haiwezekani mtu wako wa karibu anaaribu soko lake na nyie mkawa mnamwangalia tu..
 
Kwahiyo unataka sisi mashabiki tufanyeje?

Ukiona wimbo mbaya ujue wewe sie mlengwa na haujaimbiwa wewe..tuliza kipago mzee!!
 
Mara nyingi ndoa huja na mabalaa yake. Waliooa karibuni watakua wamenielewa
 
Back
Top Bottom