Ali Kiba Fans' Special Thread...

Ali Kiba Fans' Special Thread...

Na hakuna hasara pia....kwani Kiba si ndo tushamchagua??
Wenye hila za kunyea unga ili watu wasile na wapite kushotoooo!

Watapitaje kulia sasa na sisi ndio tupo huko???kila kitu tunaanza sisi wao wanafuata...nasubiri waanzishe thread yao...
Nakuambia watu roho zinawauma kutuona tunampenda Kiba hatariiii
 
Da mimi nashangaa mashabiki wa mwimba playback wameshindwa kumpigia kura king wao wa playback wa East Afrika.
 
Da mimi nashangaa mashabiki wa mwimba playback wameshindwa kumpigia kura king wao wa playback wa East Afrika.

Anawezaje kuwashinda saut soul jamani???uwezo huo hana watu wanataka mziki mzuri sio viduku
 
Diamond na Kiba wote ni wasanii wa kitanzania. Ninyi mnaojiita wapenzi, mashabiki, washangiliaji, na mengine. Vijana wanafanya kazi ili wajikwamue kimaisha. Acheni kuwagombanisha, acheni kuwafarakanisha, wapeni ushauri wapendani. Msiwe na roho mbaya kiasi hicho ndugu zangu. Wengine humu umri wao ni Mkubwa Mara tatu au mbili kwa mondi au kiba. Kwa nini wewe MTU mzima usiwashauri hao watoto wapatane waitangaze nchi kupitia music?
 
Kuna asali na shubiri,ujana kiza na nuru....we mwana wewe mwana....

Mbona jeuri sana, ulichokifata hukupata, umekosa ulivyoacha, kwa baba yako mwana, na mama yako mwana, kwa vichache ulivyotaka na vingi ulivyoacha omamee...
 
Mbona jeuri sana, ulichokifata hukupata, umekosa ulivyoacha, kwa baba yako mwana, na mama yako mwana, kwa vichache ulivyotaka na vingi ulivyoacha omamee...

Mbona unajitesa sanaaaa omame omamee,omame haya mameee aaaeeee...
Uwiii rhumba limekoleaje???
 
Daaa kuna vituko sana humu! Mimi napenda ushindani huu uendelee mkizingatia kuto sahau kununua kazi zao!
Kule WWW.mkito.com nyimbo ya Mwana Fa feat Alikiba inaongoza kwa kupakuliwa hadi sasa!

Mtifuano wa namna hii inasaidia wasanii kuto bweteka kabisa nakujua kuwa kuna upinzani kutoka kwa wengine!

Nilitegemea Matola hapo juu kwenye thread uweke website link ya mkito.com na uwaimize mashabiki wake kununua nyimbo zake.

Hata wale wa diamond nilitegemea wafungue Uzi kuhamasisha wenzao kununua nyimbo za Dianond maana haya ya kuwasifu yanaweza yasiwasaidie kabisa lakini ambacho mashabiki mnaweza kufanya ni kununua nyimbo zao na huo ndio utakuwa upendo wa kweli na ushindani ulio na tija
Shindaneni kununua nyimbo zao!

Tafadhali msitoane macho

Link hii hapa https://mkito.com/mobile/artist-profile/alikiba/564
564
cc Matola

Muda wa kununua nyimbo za Alikiba ndo huu, kumbuka hata ukidownload wimbo wa bure Alikiba anapata kiasi fulani

Tumchangie msanii tunayemkubali

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom