Nifah
JF-Expert Member
- Feb 12, 2014
- 34,020
- 79,098
Kafie mbali huko na wewe...eti ndio tunammaliza #KingKiba anaposoma comments kama hiyo yangu niliyomsifia!Ninyi ndio mtakaommaliza Kiba kabisa, anaposoma comment kama hz likichwa linavimba anajiona yupo juu,
hakuna kitu kizuri kama kumpasulia mtu ukweli kuliko kumpa sifa za marehemu,
Kiba yuko vizuri ana talent ila ni bonge la mjeuri na mvivu wa kufa mtu... usisikie ya kuambiwa tafuta ukweli wake....yaani akiacha ujeuri na kuongeza bidii na ubunifu atakua moto wa kuotea mbali.
Ila kwa sasa Diamond Platinum yuko juu sana kwa Kiba,,, the boy has what it takes to be an International star!
lazima muelewe juhudi, kujituma na ubunifu ndio silaha ya kufanikiwa popote
Narudia tena kuweni wakweli ili mumbadilishe Kiba acheni kumsifia ujinga...kwa kufanya hivi mtaendelea kumfanya awe maarufu Tz na kwenye KTMA wakati huku sio ishu tena kwa mtu kama Ali na Nasibu ishu ni nje ya mipaka, huko hakuna mizengwe kama yetu hapa bongo
Angalieni ktk tuzo za MTV za juzi, hakuna fitna pale... na kila alieshiriki na kukosa au kupata tuzo kaondoka amerizika...no longolongo wala sijui teams...
ni uwezo halisi na ubunifu tu.
Kwani kuna lipi la uongo nililolisema? Halafu ulivyo mtupu kichwani unaponda na kusifia hapohapo.
Nilitegemea useme jambo la tofauti na nililolisema mimi ila umerudia yaleyale na kuyatia maneno ya chuki ambazo tunawajua haters kama nyie hamtupi taabu.
Kiba anajua, mimi kama shabiki wake wa damu namkubali sana.
Kuhusu kupiga hatua kila kitu kina muda wake, tumeshaanza kuuona mwanga wa kimataifa kwanini tumpigie kelele?
Kwani wakati anaanza muziki ni sisi tulioenda kumpigia kelele?
Hakuna kitu kizuri kama ustaarabu, yeye Kiba anajua anachokifanya. ..tuheshimu mipango yake na kumuombea azidi kutupa burudani na apate mafanikio vilevile.