Huyo mtoa mada mwenyewe ameonyesha yupo upande upi ila diamomd ametumia vina kama vya "-re" mfano kwenye maneno kama tetere,tembere,segere na ngedere pia ametumia vina vya "-ni" katika maneno kama tafrani na mnadani sio hivyo tu ametumia takriri kama ukiangalia ametumia neno "anadodoa" zaidi ya mara moja (sina uhakika kama anadodoa nilijua anadonoa).La mwisho pia ukiangalia upangaji wake wa beti umelifanya liweze kuimbika vizuri (ingawa kuna watu wanasema shairi(wimbo) sio lazima liimbike ili mradi tu liweze kuleta maana.Hivyo kwa upande wangu naona hapo diamond amemzidi mwenzake katika uandishi.(bila mapenzi ya ushabiki)