Ali kiba kasema hashindani na mtu

Ali kiba kasema hashindani na mtu

Kiba kipaji anacho tatizo menejiment aliyonayo haina ubavu wa kumpelekesha bali yeye ndio anawapelekesha. Kama angetambua thaman yake na kuitendea kazi angekua mbali sana
uko sahihi
ana imeneji menejiment badala yenyewe im meneji
hiihihihii
 
ALIKIBA - SITAKI MTU ANIINGILIE KATIKA MIPANGO YANGU, MIMI SISHINDANI NA MTU . . Mwanamuziki mahiri nchini Tanzania, Alikiba amefunguka na kusema kuwa yeye katika muziki wake hakuna mtu anayeshindana naye na kudai ila kama kuna watu wanataka kushindana na yeye basi atawaacha na kuendelea na mambo yake. . . Alikiba anasema katika maisha yake ya muziki hataki kuona mtu yoyote anamtoa katika njia yake, ndiyo maana watu ambao wanakuwa wakiongea ongea sana juu yake yeye na muziki wake hawapi nafasi, kwani anaamini akiwapa nafasi wanaweza kumtoa kwenye mambo ambayo yeye amekusudia kuyafanya hasa zaidi katika muziki wake. "Unajua kila binadamu ana tabia yake, kuna wengine wanajua kabisa kwamba wanakosea lakini wanafanya hivyo kwa sababu na wapo wengine wanakuwa wanaongea pasipokujua kama wanakosea, hivyo mimi kama msanii sitakiwi kusikiliza hivyo vitu sababu nakuwa na mipango na malengo yangu, hivyo sitaki mtu yoyote aniingilie kwenye mipango yangu kwa hiyo ukiwafuata unaweza kujiangusha" alisema. Mbali na hilo Alikiba amesema yeye haangalii ushindani na wala hashindani na mtu . . . "Mimi siangalii ushindani na wala sishindani na mtu ila kama wapo wanashindana na mimi nitawaacha washindane na mimi lakini mimi sishindani ila naangalia malengo yangu na mipango yangu katika muziki" aliongeza Alikiba. . . TOA MAONI YAKO HAPA
Angeenda tu asainiwe na WCB if you cant beat them join them... sio dhambi..
 
Huyu Mtu najaribu kujilazimisha kumpenda na kumkubali lakini roho yangu inakataa katakata sijui ni kwanini Wajameni.
Hana jipya hapendeki jamaa mvivu sana uswahili umemzidi akiishiwa ndo akili ya kuandika mistari inarudi
 
Back
Top Bottom