Ali Kiba kortini matunzo ya mtoto

Ali Kiba kortini matunzo ya mtoto

PAZIA 3

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
1,102
Reaction score
1,919
Mzazi mwenza wa msanii Ali Kiba, Hadija Hassan amefungua kesi ya madai dhidi ya msanii huyo baada ya kumtelekeza tangu mwaka 2017.

Kesi hiyo imefunguliwa katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kwa msaada wa Kituo cha wanawake cha kisheria WLAC ambapo dada huyo anadai kulipwa milioni 1.41 ikiwemo matunzo(460,000) na ada kwa mtoto(950,000).

Dada huyo kabla ya kwenda mahakamani aliwahi kulalamika kwenye mtandao wa Instagram na ku-expose SMS kati yake na Ali zikionesha Ali akimjibu (kwa dharau) kuwa kama anataka matunzo ampeleke mtoto nyumbani kwao Ilala.

Hadija alionesha kukataa suala hilo akidai nyumbani kwa mama Ali si sehemu salama kwa mwanae wa kike sababu nyumba iko karibu na gereji bubu kadhaa na ni nyumba ya jumuiya ambapo kila mtu anaingia wakati wowote na kuhofia mwanae kutendewa vitendo visivyofaa.

Zabibu Kiba ambaye ni dada wa Ali alijitokeza na kumshukia dada huyo akisema kwao si nyumba ya jumuiya kama inavyosemwa na kwamba siku zote mtoto amekuwa akienda likizo hapo na mama yake hajawahi kulalamikia hilo.

Zabibu alienda mbali zaidi na kusema mbona mama huyo anakataa kufanya DNA kama ilivyotakiwa ustawi wa jamii? Na kwa nini alimwambia mtoto kuwa ana baba mwingine na Ali si baba yake?
 
Kiba achukue mtoto wake. Kipindi hicho chote alikuwa wapi huyu mama mtoto?
 
hivi watu wanavyoropoka hizo hela inakuwaje kwani
 
Siku zote alikuwa wapi au kaona jamaa kachukua jiko ndio figisufigisu zinaanza


Kiba achukue mtoto wake. Kipindi hicho chote alikuwa wapi huyu mama mtoto?


Acheni kuchukulia kirahisi rahisi. Kiba anatakiwa athibitishe kama anatoa matunzo kwa mwanae au amuombe waongee nje mahakama. Hawezi kumchukua mtoto kutoka kwa mamaake kirahisi kama mnavyofikiria.
 
IMG_20180507_073145.jpg
IMG_20180507_073136.jpg
IMG_20180507_073128.jpg
 
kesi hizi za kijamii huishia nje ya mahakama au ustawi wa jamii


Kesi kama hii ikiamuliwa kortini mwanaume lazima ile kwako, ndio maana unatakiwa uwe mpole umuombe dada mmalizane wenyewe.
 
Sasa matunzo ya mtoto kwa miaka 5 ni shilingi laki nne? Hiyo hela nampa Mama Gaude kwa matuzi ya wiki tu. Hawa watoto wa ma-super star wa Bongo wana maisha magumu sana.
 
Back
Top Bottom