Ali Kiba kortini matunzo ya mtoto

Ali Kiba kortini matunzo ya mtoto

Hii 1.41 ndiyo kitu gani labda?
Mlandula akili zako zinawaza odds nn. Hiyo ni odds ya kiba kumlea mwanae. Sifa ya odds 1.41 haitoagi kabisa. So hapo mwanamke ajue hapati hata sh 10 ya matunzo
 
Mlandula akili zako zinawaza odds nn. Hiyo ni odds ya kiba kumlea mwanae. Sifa ya odds 1.41 haitoagi kabisa. So hapo mwanamke ajue hapati hata sh 10 ya matunzo
Kumbe ndivyo ilivyo?
 
Mzazi mwenza wa msanii Ali Kiba, Hadija Hassan amefungua kesi ya madai dhidi ya msanii huyo baada ya kumtelekeza tangu mwaka 2017.

Kesi hiyo imefunguliwa katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kwa msaada wa Kituo cha wanawake cha kisheria WLAC ambapo dada huyo anadai kulipwa milioni 1.41 ikiwemo matunzo(460,000) na ada kwa mtoto(950,000).

Dada huyo kabla ya kwenda mahakamani aliwahi kulalamika kwenye mtandao wa Instagram na ku-expose SMS kati yake na Ali zikionesha Ali akimjibu (kwa dharau) kuwa kama anataka matunzo ampeleke mtoto nyumbani kwao Ilala.

Hadija alionesha kukataa suala hilo akidai nyumbani kwa mama Ali si sehemu salama kwa mwanae wa kike sababu nyumba iko karibu na gereji bubu kadhaa na ni nyumba ya jumuiya ambapo kila mtu anaingia wakati wowote na kuhofia mwanae kutendewa vitendo visivyofaa.

Zabibu Kiba ambaye ni dada wa Ali alijitokeza na kumshukia dada huyo akisema kwao si nyumba ya jumuiya kama inavyosemwa na kwamba siku zote mtoto amekuwa akienda likizo hapo na mama yake hajawahi kulalamikia hilo.

Zabibu alienda mbali zaidi na kusema mbona mama huyo anakataa kufanya DNA kama ilivyotakiwa ustawi wa jamii? Na kwa nini alimwambia mtoto kuwa ana baba mwingine na Ali si baba yake?
Tatizo la Ali anatembelea nyota ya Chibu,kila anapopita chibu naye humo humo...naskia na hii nayo imepangwa teh teh teh
 
Alikiba atoe matunzo ya mtoto kwa usalama wake na akubali kuyamaliza nje ya mahakama maana case ikienda mahakamani kabisa Alikiba kamwe hatoweza kushinda.....
Halafu huyo mdogo wa Alikiba so called Zabibu ana mdomo mrefu kama rula naona anaongea sana kuzidi anaye daiwa kutia mimba ni bora anyamaze na yeye amtafute mwanaume wa kumzalisha.
Huyo binti utegemezi umemzidi...ipo siku atalianzisha tu kwa Amina binti Mombasa
 
460000? Sheria gani hiyo?
Huo mshahara was mtu kabisa.
Kama sheria iko hivo wanawake wengi wasingelea watoto eke yao
Sheria ya mtoto ipo wazi kabisa kuwa mahakama inaweza kuamua mzazi atoe matunzo kulingana na pesa anayo ingiza au hali yake ya kiuchumi...
Kiasi hichi tajwa ni kidogo kabisa hivyo mahakama ina weza kabisa kumshurutisha Ali kulipa hata million 3 kwa mwezi na katika hili nina hakika Alikiba atashindwa labda atumie busara kuomba case iondolewe na wayamalize pembeni.
 
How about four others. Nimeandika kimsisitizo. Wababa mnatufanyia vitu vibaya. Tuzae then mkaoe wengine fresh.
Kwani kuzaa mnalazimishwa? Wengine mnazaa kwa kutaka mafunzo
 
Bora hata Mondi kesi yake na Mobeto ilishikiliwa na wakili binafsi,ila hawa Kituo cha wanawake cha kisheria WLAC wanatafuta sifa,hapo utakuta huyo binti ana mawakili watatu wanamsimamia,alafu ukizangatia mlalamikiwa ana jina hapo wanaona wanachukua point tatu muhimu kutoka kwa fadhili wao.Hapo Kiba mahakamani ajiandae na yy asimamishe mwanasheria wa ukweli au akamalizane nje ya mahakama.
 
Acheni wadada wa bongo wasiolewe na hawa wasanii, hivi kidoti angezaa na kiba ingekuwaje?
 
Kwa Pesa aliyokua nayo Ali Kiba sioni kesi hapo,labda kama anataka kujitia aibu..!
Huyo Dada yake Ali Kiba naona kalivalia njuga hili jambo kama yeye ndio ametia hiyo mimba mpaka mtoto akapatikana,anajisahau kabisa kama na yeye ni mwanamke..!
 
Back
Top Bottom