Ali Kiba: Kwanini watu wanachukulia poa mimi kuwa Balozi wa WildAid wakati nipo na wakina Beckham?

Kidingi

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2012
Posts
1,872
Reaction score
1,832
Alikiba anashangazwa na jinsi watanzania na mastaa wenzake wanavyoupa uzito mdogo ubalozi wake wa shirika la Wild Aid licha ya kujumuika na mastaa wakubwa duniani kwenye kampeni ya kuzuia ujangili hususan wa tembo. Akiongea jana kwenye XXL ya Clouds FM, Kiba alisema amegundua kuwa watu wengiwanachukulia poa uteuzi huo.

Kiba amesema baada ya kuteuliwa kuwa balozi wa Wild Aid aliwatumia picha wasanii mbalimbali ili wamuunge mkono kwenye kampeni hiyo na kwamba licha ya kuwepo waliompa support, alisikitishwa na jinsi suala lake lilivyochukuliwa poa .Amesema kampeni hiyo ni kubwa kuliko watu wanavyofikiria kwa kuwa ameungana na watu mashuhuri duniani wakiwemo Yao Ming, David Beckham, Leonardo Dicaprio, Prince William, Jackie Chan, Lupita Nyong'o na wengine.

"Kwanini wale wafanye na mimi pia nikiwemo lakini watu wanachukulia poa kwanini?," amehoji Kiba. "Mimi mwenyewe nimejitolea, akina Lupita Nyong'o wamejitolea watu wanachukulia poa,kwanini wanachukulia poa?

Alikiba amesema alichogundua ni kuwa Tanzania kuna tabia ya kutopeana support na kwamba tunapenda kuponda zaidi pale mtu anapofanya vibaya. "Mengi tumeyaona, marehemu Kanumba alikosea kidogo kwenye Big Brother watu wakatafuta lile walilokosea kulipublish lakini sio vile alivyoenda kutuwakilisha."

Muimbaji huyo wa Chekecha Chekechua amesema kila mmoja anapaswa kuwa mzalendo na kurejesha desturi ya kusaidiana.


Chanzo: Bongo5

==========

My take: Muosha huoshwa lakini wajifunze na wao kupeana support kuanzia kiba na wasanii wote, mbona mwenzao millen amepata tuzo bet lakini hajapewa pongezi kama inayostahili, kama ni kufanya kazi na wakina beckam, mbona diamond anaenda kuperform na wakina neyo na young thug mtv mama ye haja support..? Akumbuke tu kuwa kuna watu wanafki sana hii dunia, kwenye KTMA alipata support kubwa saana na asilimia kubwa haikuwa mapenzi ya kweli kwa kiba but njia pekee ya kumkomoa Diamond... (mfano mzuri wema sepetu-hajampost na chekecha wala ubalozi kwasababu hakuna mashindano na Diamond hapo)

Tutoane tu ujinga watanzania wenzangu, kuna mambo ya kupeana support ya kweli hata kama kuna tofauti kati yetu.. Najuwa kama ilivyo wapuuzi wachache wanavyopenda Tanzania ishindwe na wakina Davido, kuna wapuuzi wanapenda kiba nae asifanikishe campaign ya tokomeza ujangili... Huu upuuzi utokomee kwenye vitu vya msingi kama hivi basii.. #tokomezaujangili #muendemkapigekuramtvmamakwadiamondnaVanessa
 
Huko mwisho unafiki tu umeandika

kama alivyo mnafiki yeye hawapost wenzake, asipopostiwa yeye analalamika.. Ameona support anayopewa Diamond mtv mama anaona gere..

Huo ni upande mmoja wapili ni kwamba tuweke mbele mambo ya kitaifa, tutokomeze ujangili huku tunawapigia kura diamond na vanessa mtvmama... kama ulifuatilia awards za mwaka jana mtv davido baada ya kushinda artist of the year alisema ""this is for my country Nigeria"" vivyo hivyo clarence peters baada ya kuchukua best director INAUMA SANA WATU KUWEKA UPUUZI MBELE TUNASAHAU KWAMBA TAIFA LINATEGEMEA HIVI VITU, KAMA UMEMSIKIA MH. RAIS KIKWETE JANA ALISEMA SANAA YA MUZIKI INAITANGAZA NCHI PALE AMBAPO MPIRA MIGUU UNABORONGÀ afu lijitu linawaza ni diamond ndio aliye kwwnye ile category, badala ya kuwaza kuwa ni Tanzania tuliopo kwenye ile category..
 
Mungu atusaidie tu jamani mi nshachoshwa na hizi haterate!!! Pale vichwa vyao vitakapo kaa sawa na kuondoa hizi nyufa ambazo wameshazcreate kwenye jamii, hapo ndipo mambo yatakaporud kwenye msitari.
 
Kwa hyo alitakaje? Tumfate kila anakokwenda? Au tumpe support ipi?
Ally k hajielewi wala haelewi ubalozi alopewa unamaana gani....
Yeye anatakiwa apeleke kampeni hyo ya kutokomeza mauaji ya tembo and other wildlife katika maeneo yanayozunguka hfadhi jwa nchi nzima na kuwapa watu elimu juu ya madhara ya uuaji wa tembo na jinsi ya kuwatunza wanyama poli na angechapisha majarida then angeomba watu wamsupport kwa kuambatana nae kila anakokwenda kutoa elimu na katika mikutano yake na pia angeomba support ya kifedha i mean watu wamchangie then akiona watu wanamdharau au kukataa kutoa support ndo angesema hayo aliosema,
sasa ye yupoyupo tu eti balozi afu hakuna anachokifanya afu anataka support,support gani kwa mfano? Tumbebe? Au tukapge kelele barabarani. Teh teh teh kuongea bila kufikiri unachotaka kuongea ni uchizi pia.
 

umenena mkuu
 
Niliwahi kusema hili, hizi chuki za kambi zina maslahi kidogo kuliko hasara. Kutokana na chuki iliyopandikizwa, si rahisi shabiki wa Chibu kumsupport Ali. Zomea zomea za fiesta na chuki za KTMA ndizo zimechochea haya.

Way forward, ni wakati sasa wa kuweka .utanzania mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…