Alikiba anashangazwa na jinsi watanzania na mastaa wenzake wanavyoupa uzito mdogo ubalozi wake wa shirika la Wild Aid licha ya kujumuika na mastaa wakubwa duniani kwenye kampeni ya kuzuia ujangili hususan wa tembo. Akiongea jana kwenye XXL ya Clouds FM, Kiba alisema amegundua kuwa watu wengiwanachukulia poa uteuzi huo.
Kiba amesema baada ya kuteuliwa kuwa balozi wa Wild Aid aliwatumia picha wasanii mbalimbali ili wamuunge mkono kwenye kampeni hiyo na kwamba licha ya kuwepo waliompa support, alisikitishwa na jinsi suala lake lilivyochukuliwa poa .Amesema kampeni hiyo ni kubwa kuliko watu wanavyofikiria kwa kuwa ameungana na watu mashuhuri duniani wakiwemo Yao Ming, David Beckham, Leonardo Dicaprio, Prince William, Jackie Chan, Lupita Nyong'o na wengine.
"Kwanini wale wafanye na mimi pia nikiwemo lakini watu wanachukulia poa kwanini?," amehoji Kiba. "Mimi mwenyewe nimejitolea, akina Lupita Nyong'o wamejitolea watu wanachukulia poa,kwanini wanachukulia poa?
Alikiba amesema alichogundua ni kuwa Tanzania kuna tabia ya kutopeana support na kwamba tunapenda kuponda zaidi pale mtu anapofanya vibaya. "Mengi tumeyaona, marehemu Kanumba alikosea kidogo kwenye Big Brother watu wakatafuta lile walilokosea kulipublish lakini sio vile alivyoenda kutuwakilisha."
Muimbaji huyo wa Chekecha Chekechua amesema kila mmoja anapaswa kuwa mzalendo na kurejesha desturi ya kusaidiana.
Chanzo: Bongo5
==========
My take: Muosha huoshwa lakini wajifunze na wao kupeana support kuanzia kiba na wasanii wote, mbona mwenzao millen amepata tuzo bet lakini hajapewa pongezi kama inayostahili, kama ni kufanya kazi na wakina beckam, mbona diamond anaenda kuperform na wakina neyo na young thug mtv mama ye haja support..? Akumbuke tu kuwa kuna watu wanafki sana hii dunia, kwenye KTMA alipata support kubwa saana na asilimia kubwa haikuwa mapenzi ya kweli kwa kiba but njia pekee ya kumkomoa Diamond... (mfano mzuri wema sepetu-hajampost na chekecha wala ubalozi kwasababu hakuna mashindano na Diamond hapo)
Tutoane tu ujinga watanzania wenzangu, kuna mambo ya kupeana support ya kweli hata kama kuna tofauti kati yetu.. Najuwa kama ilivyo wapuuzi wachache wanavyopenda Tanzania ishindwe na wakina Davido, kuna wapuuzi wanapenda kiba nae asifanikishe campaign ya tokomeza ujangili... Huu upuuzi utokomee kwenye vitu vya msingi kama hivi basii.. #tokomezaujangili #muendemkapigekuramtvmamakwadiamondnaVanessa