Ali Kiba: Kwanini watu wanachukulia poa mimi kuwa Balozi wa WildAid wakati nipo na wakina Beckham?

Ali Kiba: Kwanini watu wanachukulia poa mimi kuwa Balozi wa WildAid wakati nipo na wakina Beckham?

Alikiba anashangazwa na jinsi watanzania na mastaa wenzake wanavyoupa uzito mdogo ubalozi wake wa shirika la Wild Aid licha ya kujumuika na mastaa wakubwa duniani kwenye kampeni ya kuzuia ujangili hususan wa tembo. Akiongea jana kwenye XXL ya Clouds FM, Kiba alisema amegundua kuwa watu wengiwanachukulia poa uteuzi huo.

Kiba amesema baada ya kuteuliwa kuwa balozi wa Wild Aid aliwatumia picha wasanii mbalimbali ili wamuunge mkono kwenye kampeni hiyo na kwamba licha ya kuwepo waliompa support, alisikitishwa na jinsi suala lake lilivyochukuliwa poa .Amesema kampeni hiyo ni kubwa kuliko watu wanavyofikiria kwa kuwa ameungana na watu mashuhuri duniani wakiwemo Yao Ming, David Beckham, Leonardo Dicaprio, Prince William, Jackie Chan, Lupita Nyong’o na wengine.

“Kwanini wale wafanye na mimi pia nikiwemo lakini watu wanachukulia poa kwanini?,” amehoji Kiba. “Mimi mwenyewe nimejitolea, akina Lupita Nyong’o wamejitolea watu wanachukulia poa,kwanini wanachukulia poa?

Alikiba amesema alichogundua ni kuwa Tanzania kuna tabia ya kutopeana support na kwamba tunapenda kuponda zaidi pale mtu anapofanya vibaya. “Mengi tumeyaona, marehemu Kanumba alikosea kidogo kwenye Big Brother watu wakatafuta lile walilokosea kulipublish lakini sio vile alivyoenda kutuwakilisha.”

Muimbaji huyo wa Chekecha Chekechua amesema kila mmoja anapaswa kuwa mzalendo na kurejesha desturi ya kusaidiana.

Chanzo: Bongo5

==========

My take: Muosha huoshwa lakini wajifunze na wao kupeana support kuanzia kiba na wasanii wote, mbona mwenzao millen amepata tuzo bet lakini hajapewa pongezi kama inayostahili, kama ni kufanya kazi na wakina beckam, mbona diamond anaenda kuperform na wakina neyo na young thug mtv mama ye haja support..? Akumbuke tu kuwa kuna watu wanafki sana hii dunia, kwenye KTMA alipata support kubwa saana na asilimia kubwa haikuwa mapenzi ya kweli kwa kiba but njia pekee ya kumkomoa Diamond... (mfano mzuri wema sepetu-hajampost na chekecha wala ubalozi kwasababu hakuna mashindano na Diamond hapo)

Tutoane tu ujinga watanzania wenzangu, kuna mambo ya kupeana support ya kweli hata kama kuna tofauti kati yetu.. Najuwa kama ilivyo wapuuzi wachache wanavyopenda Tanzania ishindwe na wakina Davido, kuna wapuuzi wanapenda kiba nae asifanikishe campaign ya tokomeza ujangili... Huu upuuzi utokomee kwenye vitu vya msingi kama hivi basii.. #tokomezaujangili #muendemkapigekuramtvmamakwadiamondnaVanessa

Ubalozi huu ni wakujitolea..hata vannesa mdee ni balozi pia kama mmeona tangazo lake..
 
Halafu hajui kujieleza kabisa... Kwenye daladala walimpiga maswali ya maana ye anajibu easy easy tu

Hakuna kitu pale!yuko kawaida mnoo,mashabiki wake wanaomsifia kwa kila kitu wanampoteza kiba,anajiona anapendwa sana na hajui kama wengi hawampendi ila wako upande wake kwa sababu wanawivu na diamond tu
 
hivi na ile kiki ya kutembelea daladala mbona kama na yenyewe haikumature??
Ile ya daladala ilibuma kabisa kama kawaida! Anacho nishangaza King ni kushindwa kusema aliihitaji nini kutoka kwetu!
Alikiba alikwenda mbali zaidi akampost Vannesa watu wampigie kura lakini akamuacha Diamond! Sasa nimeamini kuwa Alikiba ana tatizo binafsi na Diamond! Nilitegemea kutokana na upepo asinge jihusisha kabisa kwenye kupost mtu yeyote au kuongelea lolote kuhusu MTV awards!
Hivi katika ili anategemea nini?
 
Hakuna kitu pale!yuko kawaida mnoo,mashabiki wake wanaomsifia kwa kila kitu wanampoteza kiba,anajiona anapendwa sana na hajui kama wengi hawampendi ila wako upande wake kwa sababu wanawivu na diamond tu
Teh Teh...
 
naambiwa kahama Leo asubuh cunajua mwenzetu makazi rasmi bado sana,afu bado ambassador wenyw wakujitolea..mmhh! me yangu macho..?!
Bado yupo kwao imeshindikana kuhama hadi siku nyingine...
 
Teh Teh...

ahahaha!!halfu alivyo kilaza anasema eti" watu wananipenda sana kuzidi mwanzo,sasa hivi nimekua na mshabiki wengi sana!"
Hajui kwanini watu wengi wanaigiza kumpenda?!

Wengi waliomshindwa daimond mfano Ommy wamekimbilia kwa king kuunganisha nguvu za kiushindani,wenye chuki wote karata yao ya mwisho ni allykiba kwa diamond,nayenyewe inaelekea kushindwa kabisaa
 
Kweli sisi wabongo hatujiekewi, wanigeria when it comes to national interest itikadi zinawekwa pembeni, sijui tunakula maharage ya wapi sisi, tunaua mziki wetu bila kujua wakati ushatake over, huu mtindo Wa kuvutana shimoni Kwa aliyetoka unatufanya tuwe average people in front of others wakati we gat many potential infront of us, tubadilike!!
 
Na hili jambo ndilo huwa linanishangaza na haliwezi kumsaidia kabisa..
 
Kweli sisi wabongo hatujiekewi, wanigeria when it comes to national interest itikadi zinawekwa pembeni, sijui tunakula maharage ya wapi sisi, tunaua mziki wetu bila kujua wakati ushatake over, huu mtindo Wa kuvutana shimoni Kwa aliyetoka unatufanya tuwe average people in front of others wakati we gat many potential infront of us, tubadilike!!
Mkuu kuwa clear nina anavyuta shimoni na nani au ninani ana mvuta mwenzie shimoni? Unafikiri ili swala linatakiwa kumalizwa na nani?
 
Thubutuu!JOJO si anapesa aende akakae kwake,yaani daladala tour imenichekesha sana
Jojo sidhani kama anampenda nina hakika ni kutaka kumkomesha Diamond na kutafuta kick tuu...
 
Halafu huo ubalozi wenyewe mi nilijua amechaguliwa kati ya maelfu!!kumbe ni kazi ya kujitolea tu?!!
Yani anaona ajitoleee kabisa? amelidhika na nini? Yeye ana jifananisha na wakina Jackline Mengi ambao kwao pesa si tatizo? Siamini kabisa kama anafanya kazi hii bure kabisa ...Hakika nitaendelea kushangaa ...
 
Kiba angekua ana akili au washauri wazuri angeomba collabo na diamond ili atoke tena kimziki na sio kutaka kushindana na mtu aliyemzid kila kitu kwasasa. Tatizo mashabiki wake wanamtia ujinga kwakumwambia yeye anajua kuliko diamond which is far away to be true!
 
Back
Top Bottom