Ali Kiba: Mkataba wangu na Sony Music hautanifanya nikae kimya kwenye muziki

Ali Kiba: Mkataba wangu na Sony Music hautanifanya nikae kimya kwenye muziki

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
Kama ulidhani Alikiba atapotea kwenye ramani ya muziki baada ya kusaini mkataba na kampuni ya Sony Music kama ilivyowahi kuwatokea baadhi ya wasanii wa Afrika – imekula kwako, mwenyewe amefunguka.

Hitmaker huyo wa ‘Aje’ amekiambia kipindi cha 255 cha Clouds FM, Alhamisi hii kuwa hawezi kukaa kimya zaidi ya miezi mitatu bila ya kuachia nyimbo mpya kitu ambacho amedai kitamfanya awe juu zaidi.

“Nimejiandaa vizuri na pindi unapokuwa unasaini kitu, ina maana kuwa umekubaliana na kila kitu, kwa hiyo mimi pia ninamatakwa yangu na hata wao pia wanamatakwa yao. Kwa hiyo kitu ambacho kipo hapo ni kwenda na agreement. Mimi siwezi kukaa muda zaidi ya miezi tatu bila kutoa ngoma na huo ndio mkataba wangu jinsi unavyosema,” alisema Alikiba.

Muimbaji huyo alifanikiwa kusaini mkataba na kampuni hiyo mwezi Mei mwaka huu na tayari ameshafanikiwa kuachia wimbo mmoja mpaka sasa akiwa chini ya kampuni hiyo.

1478266468720.png

"Yooooooooh"
 
Hongera yake, na kiukweli kimuziki unakuja vizuri ipo siku moja utakuja kuwa juu kama DIAMOND,lakini kwasasa bado sana tena sana. Maana hata shoo zako zinaishia Mombasa tena nazo ni kwa offer ya Gavana unayejuana nae,sivizungumzii vitu vingine ulivyopitwa na DIAMOND maana inajulikana ila mashabiki wako wanakujaza ujinga.
 
Lakini toka ame sign kaachia wimbo mmoja tuu.
Hao Sony bado si watu wazuri wasanii wengi sana wamepotelea huko.
Kwa sasa bora hata mtu uwe WCB, Sony hawaaminiki
 
Kama mkataba unampa uhuru wa kutoa ngoma kadri anavyojisikia basi fine lakini kama kila kitu kinakuwa regulated na Sony, basi anatakiwa kufikiria kauli zake mara mbili mbili kwa sababu hata hao akina Davido ambao walikuwa wanakaribia kumaliza mwaka sio kwamba hawakuwa na uwezo wa kutoa kazi wao kama wao.
 
Hongera yake, na kiukweli kimuziki unakuja vizuri ipo siku moja utakuja kuwa juu kama DIAMOND,lakini kwasasa bado sana tena sana. Maana hata shoo zako zinaishia Mombasa tena nazo ni kwa offer ya Gavana unayejuana nae,sivizungumzii vitu vingine ulivyopitwa na DIAMOND maana inajulikana ila mashabiki wako wanakujaza ujinga.

Sio kwa ukweli huo hahahhahah.. Tatizo wakija wataipibga hadi hii kauli yako..
 
Back
Top Bottom