Mkuu
pwilo,
Umekosea sana kumuhusisha Simba na tofauti iliyopo kati ka kiba na aby daddy! (Kama tofauti zao zimekuwa kubwa kiasi hicho)
Kuhusu wimbo wa kokoro:
Wimbo huu haujarekodiwa juzi juzi kama unavyodhani.. Wimbo umerekodiwa kabla mavoko hajamwaga wino rasmi wcb (ndio walikuwa kwenye mazungumzo)
Kwahiyo kipindi mavoko ameingia rasmi wcb tayari alikuwa na huu wimbo ukiwa umeingizwa verse moja tayari na ulikuwa na chorus tofauti kidogo na hii chorus ya sasa (zinafanana kidongo ingawa).
Na ieleweke kuwa mavoko pia anazo nyimbo nyingine nyingi hazijatoka zimerekodi kabla hajaingia wcb!
So miezi kama miwili iliyopita baada ya kukubaliwa kuwa wimbo huu utoke na kufanyiwa video, kilichofanyika ni kuurekebisha kiasi na kuuboresha... Ndio hapo Simba akaingiza verse yake na kuingiza sauti kwenye chorus.. Kisha Laizer akaujazia vionjo vichache na kuufanyia 'mastering'..
Hicho ndicho kilichofanyika..
Si sawa kumuhusisha Diamond na kila kitu cha Kiba kinachoenda kombo!
Kwa niaba ya mashabaki wote wa Diamond platnumz na WCB, tuwaoombee heri Kiba na Abby Daddy wafikie muafaka na waendelee na kazi.. Tunahitaji wasanii wengine waongezeke kuiwakilisha Tanzania kimataifa! Kiba kukosana na Abby daddy ni setback na sio suala linalosogeza mziki wetu..
The Bold.