Ali Kiba na Millard Ayo washuhudia uzinduzi wa Phantom 6

Ali Kiba na Millard Ayo washuhudia uzinduzi wa Phantom 6

TECNO Tanzania

Senior Member
Joined
Jul 6, 2016
Posts
192
Reaction score
217
Hatimaye Tecno wamezindua Phantom 6 na Phantom 6 Plus ambazo zinaleta mapinduzi ya Teknolojia

Kampuni inayoongoza kwa mauzo ya simu Afrika, Tecno Mobile imezindua simu mbili matata za Phantom 6 na Phantom 6 Plus katika tukio lililohudhuriwa na watu maarufu kibao katika Hotel ya Armani ambayo ipo katika jengo refu zaidi duniani “Burj Khalifa”. Uzinduzi huu umefanyika wakati ambapo kampuni ya Tecno inatimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake.

ANGALIA KIPANDE KIFUPI CHA VIDEO YA TECNO PHANTOM 6

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi amesema “Imetuchukua takribani miaka 3 katika matengenezo yake na imehusisha zaidi ya wahandisi laki 5” amesema Mkuu wa Masoko wa Tecno, Vane Ni

"TECNO Phantom 6 inawapa watumiaji wa simu za mkononi utulivu bora pindi wanapotumia, kasi na kamera bora na nzuri ili kufurahia zaidi simu ya mkononi” amesema Naibu Kiongozi wa Masoko wa Tecno Nigeria, Attai Oguche.

Uzinduzi ulifana sana ambapo kulikuwa na zaidi ya vyombo vya habari 70 tofauti kutoka chini mbalimbali duniani kote na miongoni mwa mastaa waliohudhuria ni mwanamuziki mahiri wa Tanzania, Ali Kiba na mwanahabari “Mtu wa Nguvu Millard Ayo ambaye alishinda safari ya kwenda China.

3.PNG

Pichani ni mwanahabari wa Tanzania Millard Ayo akitangazwa mshindi wa Safari Safari ya China.

4.PNG

Mwanamuziki wa kimataifa wa Tanzania, Ali Kiba akiwa na kifaa kipya cha Phantom 6 akifanya mauzungumzo.

Baada ya uzinduzi huo Tecno Tanzania ikatangaza kwamba Phantom 6 na Phantom 6+ zitaanza kupatikana rasmi kuanzia tarehe 8 Oktoba 2016 katika duka la Tecno lililopo City Mall Posta ambapo wateja wote watakaonunua Phantom 6 siku hiyo watapatiwa vifurushi vya zawadi na kutakuwa na zawadi kubwa nono. Pia wakatangaza kwamba kuanzia Jumatatu tarehe 3 Oktoba wateja watajaza fomu maalum ili kuweka oda zao na watazawadiwa zawadi mbalimbali zikiwemo T-Shirts, mabegi, T-Band na Sefie stick siku ya kuanza mauzo hiyo tarehe 8 Oktoba. Kuhusu bei kwakweli Tecno wameangalia hali halisi ya uchumi kwa sasa ambapo gharama itakuwa kati ya Tsh 500,000 - Tsh 600,000.

TOFAUTI KATI YA PHANTOM 6 NA PHANTOM 6+

upload_2016-9-29_19-19-58.png

Kwa taarifa zaidi unaweza kutembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya Tecno na hakikisha hukosi mojawapo ya simu hizi kali ambazo zimekuja kufanya mageuzi ya teknolojia.

Facebook: TECNO Mobile | Facebook

Instagram: TECNO Mobile Tanzania (@tecnomobiletanzania) • Instagram photos and videos

Twitter: TECNO Mobile TZ (@TECNOMobileTZ) | Twitter
 
Tecno walete mapinduzi gani ya maana. Kesho watatoa phamtom 8 hata cku haijaisha
 
Millard Ayo hizo swaga za earphones ushamba sasa.
Upo ktk stage kubwa unatangazwa mshindi huku umevaa earphone?

Anyways... Matoleo ya Tecno kila uchwao yamenikumbusha member mmoja humu alisema "Ukinunua Tecno toleo la mwisho ukifika nyumbani kabla hujamalizia kuichaji wameshatoa toleo jingine"
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Yupo anatangaza Amplifaya
 
Aahh Niffah leo umezingua
 
Swali la kichokozi;
Hivi mnaubia na yule TEKNO msanii wa Nigeria?
 
Back
Top Bottom