Wengi wanadhani mwanamziki Ali Kiba hapendi makuu au hapendi kujionyesha, lakini hili si kweli. Huyu mwanamziki kwanza ni mbinafsi sana, ana majivuno na mwenye wivu sana. Mifano ni mingi kuonyesha haya mambo hasi kwake.
1. Mjivuni: ukimwangalia tu, kwa kuongea kwake, majibu yake anapoulizwa maswali na mikogo yake, unaona kabisa huyu mtu ni mjivuni sana. Ali Kiba anataka aonekana kuwa yeye ni kila kitu, lakini zaidi ya sauti nzuri aliyokuwa nayo, hana kitu kikubwa ambacho anaweza kujivunia nacho.
2. Mbinafsi: Nashindwa kuelewa ni vipi mwanamziki aliyekuwepo kwenye muziki zaidi ya miaka 15, eti leo ndio anakuja na music label kisa tu mpinzani wake anayo. Kama kweli wewe ni King, hivi vitu ulitakiwa uwe umevifanya miaka mingi iliyopita ili kusaidia vijana chipukizi na sio ufanye kwa ajili ya kushindan na mpinzani wako.
Katika miaka yake yote kwenye muziki, ukiacha wasanii wake wa King's Music, sijasikia msanii yeyote ambaye anaweza kutoka mbele ya jamii na kusema Ali Kiba amemsaidia kwenye muziki.
3. Mwenye wivu sana: Hili halina ubishi, Ali Kiba anamuonea wivu sana Diamond. Angependa sana awe kama yeye lakini anajua kabisa hawezi. Kuimba ni kitu kimoja, lakini huu mziki ni zaidi ya kuimba. Kuna kuburudisha (entertainment), kuna showbiz, kuna bidii ya kazi, na pia kuna biashara. Ali Kiba ana kimoja tu, ambacho ni kuimba tu, hivyo vingine hana. Na bahati mbaya Diamond ndio hapo anapopata nafasi ya kuwa bora.
LEO KWELI KWENYE JAMII YA DIGITAL NA SOCIAL MEDIA, HUWEZI UKASEMA FUN BASE YA MTU KWENYE SOCIAL MEDIA NI KITU KIDOGO. Eti kuna wale watu wanasema views za You Tube sio lolote. Views za You Tube ndio biashara hiyo, hilo ndio soko la mwanamuziki kwa sasa. Wingi wa fan base ndio husambaza bidhaa ya mwanamuziki. Ndio maana leo hata Diamond akitoa nyimbo mbaya vipi na Ali Kiba atoe nyimbo nzuri sana, bado Diamond atauza zaidi nyimbo yake kwa kuwa soko lake ni kubwa na analijua linataka nini.
Kwa kumalizia, MUZIKI SIO SIFA, MUZIKI NI BIASHARA.