Ali Kiba ni mjivuni, mbinafsi na mwenye wivu sana

Wengi wanadhani mwanamziki Ali Kiba hapendi makuu au hapendi kujionyesha, lakini hili si kweli. Huyu mwanamziki kwanza ni mbinafsi sana, ana majivuno na mwenye wivu sana. Mifano ni mingi kuonyesha haya mambo hasi kwake.

1. Mjivuni: ukimwangalia tu, kwa kuongea kwake, majibu yake anapoulizwa maswali na mikogo yake, unaona kabisa huyu mtu ni mjivuni sana. Ali Kiba anataka aonekana kuwa yeye ni kila kitu, lakini zaidi ya sauti nzuri aliyokuwa nayo, hana kitu kikubwa ambacho anaweza kujivunia nacho.

2. Mbinafsi: Nashindwa kuelewa ni vipi mwanamziki aliyekuwepo kwenye muziki zaidi ya miaka 15, eti leo ndio anakuja na music label kisa tu mpinzani wake anayo. Kama kweli wewe ni King, hivi vitu ulitakiwa uwe umevifanya miaka mingi iliyopita ili kusaidia vijana chipukizi na sio ufanye kwa ajili ya kushindan na mpinzani wako.

Katika miaka yake yote kwenye muziki, ukiacha wasanii wake wa King's Music, sijasikia msanii yeyote ambaye anaweza kutoka mbele ya jamii na kusema Ali Kiba amemsaidia kwenye muziki.

3. Mwenye wivu sana: Hili halina ubishi, Ali Kiba anamuonea wivu sana Diamond. Angependa sana awe kama yeye lakini anajua kabisa hawezi. Kuimba ni kitu kimoja, lakini huu mziki ni zaidi ya kuimba. Kuna kuburudisha (entertainment), kuna showbiz, kuna bidii ya kazi, na pia kuna biashara. Ali Kiba ana kimoja tu, ambacho ni kuimba tu, hivyo vingine hana. Na bahati mbaya Diamond ndio hapo anapopata nafasi ya kuwa bora.

LEO KWELI KWENYE JAMII YA DIGITAL NA SOCIAL MEDIA, HUWEZI UKASEMA FUN BASE YA MTU KWENYE SOCIAL MEDIA NI KITU KIDOGO. Eti kuna wale watu wanasema views za You Tube sio lolote. Views za You Tube ndio biashara hiyo, hilo ndio soko la mwanamuziki kwa sasa. Wingi wa fan base ndio husambaza bidhaa ya mwanamuziki. Ndio maana leo hata Diamond akitoa nyimbo mbaya vipi na Ali Kiba atoe nyimbo nzuri sana, bado Diamond atauza zaidi nyimbo yake kwa kuwa soko lake ni kubwa na analijua linataka nini.

Kwa kumalizia, MUZIKI SIO SIFA, MUZIKI NI BIASHARA.
SERIES YA KEEP UP WITH KARDASIAN YA KIBONGO INAENDELEA HUKU TUKITAZAMIA 2025 KUWA NCHI YA V-WONDER KWA KUWEPO VYOMBO HURU VYA GRAVEPINE ZAIDI YA TMZ.
 
Mugisher,

Why kiba?

Kuna wanamuziki wengi sana

Kinachowasumbua kumfuatilia huyu ni nini?
Unataka wamuongelee 20%?..vioo vya music wa Tanzania ni Mondi na Kiba hao ndio maicons wa bongofleva huwezi kuongelea Bongofleva ya sasa pasina kuwataja hao japokuwa Diamond anamfunika Kiba kwa vitu vingi
 
Zote hizo, kama ni kweli, ni haki zake za kikatiba.

Na pia, labda ndiyo sababu zimemfanya ajulikane.

Ukiwa si mbinafsi, si mjivuni na huna wivu, kabisa, huwezi kuwa star.

Kwa sababu kuwa star ni ubinafsi na ujivuni Umejiweka wewe pale juu, fans wako wako chini.

Katika sanaa, kuna aina ya sanaa inayojulikana na kukubalika kabisa ya ujivuni.

Inaitwa braggadocio. Hii ipo tangu kwenye medieval plays na Opera. Ukiliangalia hilo jina limekaa kitaliani. Rappers wanaitumia sana hii style. Ukiwa huelewi braggadocio ni nini, unaweza kufikiri hawa rappers ni vichaa, wanavyojisifia. Kumbe wanashindana sanaa ya kujisifia. Na tunaojua wanaojisifia sana hawana kiti, hata halitusumbui hili.

Ukiwa msanii wa sanaa ya Bongo fleva halafu ukashindwa kuwa mjivuni, umeshindwa hiyo sanaa.

Kwa sababu sanaa yenyewe inataka mtu mjivuni, akae juu pale.

Inataka uwe na swagger.

Unawaamrisha fans, mikono juu, mikono juu, watu wanakutii kama ng'ombe, wanarusha mikono juu.

Say yooo. Say yeee. Wanakujibu. Wanakufuatisha.

Nguvu yote hii aipate mtu mmoja, kama si ubinafsi ni nini?

Kama si ujivuni ni nini?

Bila mwanamuziki kuwa na wivu hawezi kushindana na wenzake. Wivu ndio unaleta ushindani na maendeleo.

Mwanamuziki asiye mbinafsi, mjivuni na mwenye wivu amekosea taaluma.

Alitakiwa kuwa mtawa, si mwanamuziki.
unachomaanisha si kama kile mtoa mada anacho kimaanisha! alikiba ni mtu anaejiona kamaliza ilihali ni mtu ambaye bado anastahili kufanya juhudi zaidi ili afike mbali..
 
Akili nyingi Sana hii ..big up bro

Sasa unabisha kwa kuandika kwamba ninachomaanisha si kile mtoa mada anacho maanisha, halafu unaandika kitu ambacho hakipingani na nilichoandika mimi.

Maana yake nini?

Kwani mimi nimeandika Ali Kiba ni mtu anajiona hajamaliza?

Yani kuandika kote huko mpaka braggadoccio, ambapo hujanielewa ni wapi?
 
sifa ulizoandika ni zakila mwanadam, niwenye hekima na busara2 ndo hufanikiwa kuzificha hata wewe
 
unachomaanisha si kama kile mtoa mada anacho kimaanisha! alikiba ni mtu anaejiona kamaliza ilihali ni mtu ambaye bado anastahili kufanya juhudi zaidi ili afike mbali..
Afike mbali wapi? Ili iweje? Kwanini mnataka Ali kiba awe kama diamond? Kama hapo alipofika ndio mwisho wake unataka aende wapi? Wewe mbona hujitumi ufike mbali uwe kama bakhressa au mengi? Umeridhika na maisha yako ya chumba kimoja mbagala magengeni na simu yako ya tecno pop 1 ya laki moja na nusu?
 
Pia jamaa anadharau sana nilifika kwake tabata anakokaa na wale wasanii wake majina anayowaita ni ''kiazi njoo hapa " tena mbele za watu
 
Kiba kawakamata pabaya hawaishi kumuongelea
 
Zote hizo, kama ni kweli, ni haki zake za kikatiba.

Na pia, labda ndiyo sababu zimemfanya ajulikane.

Ukiwa si mbinafsi, si mjivuni na huna wivu, kabisa, huwezi kuwa star.

Kwa sababu kuwa star ni ubinafsi na ujivuni Umejiweka wewe pale juu, fans wako wako chini.

Katika sanaa, kuna aina ya sanaa inayojulikana na kukubalika kabisa ya ujivuni.

Inaitwa braggadocio. Hii ipo tangu kwenye medieval plays na Opera. Ukiliangalia hilo jina limekaa kitaliani. Rappers wanaitumia sana hii style. Ukiwa huelewi braggadocio ni nini, unaweza kufikiri hawa rappers ni vichaa, wanavyojisifia. Kumbe wanashindana sanaa ya kujisifia. Na tunaojua wanaojisifia sana hawana kiti, hata halitusumbui hili.

Ukiwa msanii wa sanaa ya Bongo fleva halafu ukashindwa kuwa mjivuni, umeshindwa hiyo sanaa.

Kwa sababu sanaa yenyewe inataka mtu mjivuni, akae juu pale.

Inataka uwe na swagger.

Unawaamrisha fans, mikono juu, mikono juu, watu wanakutii kama ng'ombe, wanarusha mikono juu.

Say yooo. Say yeee. Wanakujibu. Wanakufuatisha.

Nguvu yote hii aipate mtu mmoja, kama si ubinafsi ni nini?

Kama si ujivuni ni nini?

Bila mwanamuziki kuwa na wivu hawezi kushindana na wenzake. Wivu ndio unaleta ushindani na maendeleo.

Mwanamuziki asiye mbinafsi, mjivuni na mwenye wivu amekosea taaluma.

Alitakiwa kuwa mtawa, si mwanamuziki.

Hili jibu ni marking scheme ya swali la PhD
 
Jf ingekuwa na watu wenye akili kama we we hadhi yake ya zamani ingerudi tatizo imevamiwa na vijana wa Facebook tunapata taabu sana
 
Ali Kiba kafanya sana kolabo na wasanii chipukizi ili watoke kimziki au unataka awasaidiaje?
Kwanza Dada yake mondi queen darling kamsaidia kweli kimuziki, wakati kaka yake bado hajulikani, Leo hii kajulikana kaka yake kampotezea kiba, mleta posti naona hajui hili, anayemsifia kwanza kazi yake kuwatangaza watu ila mchoyo kuwapa maisha wenzake, wafatilie wote waliotoka kwake.
 
kiba ni wa kusaidiwa na queen darlin kwa sasa kweli[emoji1787][emoji1787]
 
Hizo ndio tabia za waha kule kigoma muha akifanikiwa kidogo anakua msumbufu sana
 
Swali la msingi ,kwanini azungumziwe Alikiba?wangapi aliwakuta kwenye mziki,wangapi alianza nao, wangapi walianza baada yake,?bado kiba anauwezo mkubwa ila kiukweli kazidiwa umaarufu na mbinu za kibiashara japo na yeye analifahamu na ili uelewe mbinu yake ipo imara zaidi ni kwamba haufuati mkumbo fikiria vizuri .Tatizo1 tu hit zilizoshiba japo2 kwa mwaka hilo ndo hitaji kubwa la soko
 
Back
Top Bottom