Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
ALI MSHAM, JULIUS NYERERE NA WANACHAMA WA TANU WA TAWI LA MTAA WA JARIBU MAGOMENI MAPIPA 1954
Watoto wa Ali Msham walizihifadhi picha hizo hapo chini kwa zaidi ya miaka 60.
Miongo sita imepita hadi picha hizi kufika mikononi kwangu na ndiyo ikawa sababu ya historia ya Ali Msham mzalendo aliyefungua moja ya matawi ya kwanza ya TANU yaliyokuwa na nguvu kufahamika.
Nyumba palipofunguliwa tawi hili Mtaa wa Jaribu ipo hadi leo na wanae wanaishi katika nyumba hii.
Kwa namna ya kushangaza nyumba hii imekuwa kivutio cha wanahabari wengi wakifika pale kuitazama.
Kinachowavutia khasa ni kuwa hapa katika nyumba hii Mama Maria alikuwa na duka lake dogo akiuza mafuta ya taa wakati yeye na mumewe walipohamia Magomeni Maduka Sita.
Kumuondolea Mama Maria adha ya kwenda Kariakoo ambako alikuwa na duka lake la kwanza la mafuta ya taa Mtaa wa Mchikichi na Livingstone, Ali Mshama alimfungulia duka hapo nyumbani kwake.
Pamoja na duka hili la Mama Maria Ali Msham alifungua shule ya TAPA upande mmoja wa nyumba yake wasome watoto wadogo wa masikini (shule hizi zilizokuwa zikimilikiwa na Tanganyika African Parents Association (TAPA) zilitoa mchango mkubwa kwa watoto kusoma ambao wazazi wao walikuwa na kipato cha chini).
Ukiangalia picha ya Mtaa wa Jaribu ulivyokuwa miaka 60 iliyopita utaona nyumba zimeishia Mtaa wa Idirisa kwa sasa na kuanzia hapo kwenda mbele ni vichaka, minazi na mkorosho.
Nyakati za jioni maghrib ikiingia sehemu hiyo ilikuwa kiza.
Ali Msham alimpa kazi mmoja wa wanae jina lake Abdallah Omari Likonda kuwa anamsindikiza Mama Maria na kumbebea vitu vyake hadi nyumbani kwake.
Abdallah Omari Likonda yu hai na sasa ni mtu mzima anaishi Mvuti Chanika.
Picha ya kwanza kulia ni Ali Msham na Julius Nyerere ni huyo kakaa nyuma ya meza akiwa na wanachama wa TANU.
Siku hii Ali Msham alimkaribisha Nyerere tawini ili amkabidhi samani aliyochonga kwa ajili ya ofisi yake New Street.
Picha ya pili kushoto inamuonyesha Ali Msham aliyekaa kati shati jeusi na wanachama wa tawi la TANU Magomeni, picha inayofuatia ni siku wanachama wa walipokusanyika kwenye tawi kufanya dua kwa ajili ya safari ya Mwalimu Nyerere UNO 1955.
Picha ya mwisho ni hapo tawini Magomeni inamuonyesha kulia Sheikh Suleiman Takadiri, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU, kushoto ni John Rupia na katikati aliyeshika tama ni Zuberi Mtemvu; Julius Nyerere haonekani amezibwa na John Rupia.