Ali Mwakwere alipomuadhimisha Hamza Kibwana Mwapachu kwa kumpa mtaa kwale Mombasa

Ali Mwakwere alipomuadhimisha Hamza Kibwana Mwapachu kwa kumpa mtaa kwale Mombasa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
49da3588-00cc-43e9-aa96-f3873b8e3bb4

_94625529_97cddfec-0537-41df-8a6b-af4247ecf14f.jpg

Chirau Ali Mwakwere na Rais Jakaya Kikwete nyuma ni Balozi Mohamed Maharage Juma Mdigo wa Gombero.

[9:45 PM, 2/13/2017] +255 687 500 699: Huyu Ali Mwakwere ni Mdigo wa Kwale.

Siku alipokutana na Juma Mwapachu wakati ule Juma Mwapachu Secretary General EAC wakajuana kuwa wote ni Wadigo.

Juma akamuhadithia Mwakwere historia ya baba yake Hamza Kibwana Mwapachu alisoma Makerere pamoja nä Julius Nyerere.

Hamza akiwa Mdigo wa kwanza kuingia Makerere.

Mwakwere aliporejea Kwale akaiomba Council ya Kwale umpe mtaa Hamza Mwapachu kwa kuheshimu kuingia Makerere kwa Mdigo wa kwanza.

Ukienda Kwale utakuta huu mtaa - Hamza Mwapachu Street.

[9:45 PM, 2/13/2017] +255 687 500 699: Mimi nilikutana na Ali Mwakwere kwenye Maulid ya Lamu.☝

[9:45 PM, 2/13/2017] +255 687 500 699: Hapa nyumbani Hamza Mwapachu hajapewa mtaa hata kwao Tanga.

Nilimuuliza Guled Meya wa Tanga hivi nyie hamuoni vibaya kuweka jina "Maua" katikati ya mji ilhali mna mashujaa waliopigania uhuru kutoka Tanga?

Nikampa majina - Hamisi Heri, Sheikh Abdallah Rashid Sembe, Mohamed Kajembe ...
 
Meya Guled alikujibu je mzee Mohamed!
 
Mzee Said huyo Guled ndiye yule meya wa CCM aliyepatikana kimazingaombwe
 
[emoji443]zipapa zipapa[emoji443] X2
ndo wimbo alikuwa anapenda sana kuuimba huyo mbunge wa zamani wa kwale
 
nilivyoona hiz porojo za mitaa nikasema lazima utakuwa ni wewe 'msomi mwanasesere'
Mtanganyika...
Unaweza ukanipinga bila ya kunitukana na kunikejeli.

Watu daima tutakuwa na fikra zinazokinzana na hili sijambo baya.

Kisichopendeza ni kumtukana na kumkejeli mwenzako kwa kuwa
tu hukubaliani na fikra zake.

Ungeweza ukasema kuwa hukubaliani na Hamza Mwapachu kupewa
mtaa na ukatoa sababu zako ingetosha na ingekaribisha mjadala
ambao ungeleta manufaa kwa jamii.

Wanaotaka kumjua Hamza Mwapachu na umuhimu wake waingie hapo
chini:
Mohamed Said: KUTOKA JF: HUTOMSOMA MWALIMU NYERERE PEKE YAKE
Mohamed Said: WATOTO WA WAPIGANIA UHURU BI. MAUNDA PLANTAN, JUMA MWAPACHU, HAPPY MTAMILA NA KLEIST SYKES WANAPOWAKUMBUKA WAZEE WAO
Mohamed Said: KUTOKA JF:KATIBA YA TANGANYIKA 1950
Mohamed Said: HAMZA MWAPACHU, ABDULWAHID SYKES NA CHIEF MICHAEL LUKUMBUZYA
Mohamed Said: KUTOKA JF: KAULI YA HAMZA MWAPACHU KWA UONGOZI WA TAA 1953
Mohamed Said: FB: JUMA MWAPACHU AMZUNGUMZIA BABA YAKE KATIKA HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA

Kuna mtu kaniomba ruksa amtukane Mtanganyika...nimemwambia jambo
lolote ukilitia upole litapendeza.

Ukimtukana Mtanganyika na wewe utakuwa kama yeye.
Naamini hatofanya hivyo.
 
Hongera sana Mzee Said kwa uandishi wako mzuri,
Hoja yangu kwako ni kwa nini uandishi wako umeegemea upande mmoja tu?
Kina Paulo, yohana, matayo na Jeremia sikuoni ukiwataja walau kwa uchache kulikoni?
Ina maana historia yoyote katika nchi yetu haikuwa na hao watu?

Ingawa ukweli utabaki kuwa ukweli tu kuwa una uandishi unaomshawishi msomaji kupenda kuendelea kusoma makala zako.
 
Ho Chi Minh,
Nitawataje ikiwa hawakuwapo?
Pale walipokuwapo nimewataja.
 
Hongera sana Mzee Said kwa uandishi wako mzuri,
Hoja yangu kwako ni kwa nini uandishi wako umeegemea upande mmoja tu?
Kina Paulo, yohana, matayo na Jeremia sikuoni ukiwataja walau kwa uchache kulikoni?
Ina maana historia yoyote katika nchi yetu haikuwa na hao watu?

Ingawa ukweli utabaki kuwa ukweli tu kuwa una uandishi unaomshawishi msomaji kupenda kuendelea kusoma makala zako.
Ho Chi Minh,
Hebu soma hii kutoka kitabu cha Abdul Sykes:
''Mwezi June, makao makuu ya TAA yalitangaza kamati yake ya utendaji: J. K. Nyerere, Rais, Abdulwahid Sykes, Makamu wa Rais; J. P. Kasella Bantu, Katibu Mkuu; Alexander M. Tobias na Waziri Dossa Aziz, Katibu wa pamoja wa muhtasari; Wajumbe wa kamati: Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said Tewa, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo na Patrick Aoko.''
 
Back
Top Bottom