Ali Saleh Alberto alipoingia maktaba na kitabu mkononi - Zanzibari hustler

Ali Saleh Alberto alipoingia maktaba na kitabu mkononi - Zanzibari hustler

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
23,526
Reaction score
34,057
ALBERTO ATEMBELEA MAKTABA NA KITABU "ZANZIBARI HUSTLER" MKONONI

Mbele ya Ali Saleh mimi sinyanyui kalamu yangu kuandika kitu.

Isome kalamu inayokata kama wembe mpya:

"Leo nilifika kwa mwana historia na mwandishi maarufu na sahiba wangu Sk Muhammed Said mjini Dar.

Pamoja na mazumgumzo maana sisi huwa na mengi, nilimkabidhi kwa ajili ya Maktaba yake kitabu kiitwacho ZANZIBARI HUSTLER kilichoandikwa na Hamid Haji (Sampati) juu ya safari zake Afrika, Asia Ulaya, Carribian na Canada kusaka ubaharia lakini akaishia kwenye biashara haramu.

Kitabu kinaelezea juu ya uchu wa binaadamu kufanikiwa, ambapo yeye hakufakiwa na hata aliporudi Zanzibar ndipo akazama katika uteja, mpaka akakabiliwa na mashtaka ya kutumia na kusambaza mihadharati na kusota jela ya Kiinua Miguu mwaka nzima.

Kadhia nzima imehadithiwa vyema kwa kalamu yake..kwenye safari zake za Pakistan. Italia, Misri, Sudan, Afrika ya Kati, Gabon. Cameroon, Guinea Bissau, Guinea Conakry na Ivory Coast akidandia usafiri huu na ule.

Kisha pia akadandia meli hadi Spain ambako alifanya mzamio kufuata unga Colombia na kutopea kwenye unga ndani ya nchi hio ya Spain.

Akailenga Canada kupitia Cuba ambako akaishi miaka miwili kabla kurejeshwa kwao Zanzibar.

Hamid ni mpishi mzuri na anaezumgumza Kihispaniola, Kiingereza na Kireno na aliwahi kuoa na ana watoto wawili.

Ikumbukwe tu safari yake ya mwanzo alikuwa na miaka 17 na passppoti ya kudanganya umri.

Kitabu kinapatikana Mkuki na Nyota, Dar es salaam na pia Masomo Bookshop, Unguja"

1770241045541.png
 
Back
Top Bottom