Mtani wa Taifa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2023
- 953
- 3,318
Ewe rafiki yangu rudi nyumbani mkeo anaumwa achana na mchepuko huo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wacha akitulia atasema alitoa ngapi na huko zimebaki ngapi!Hapo mshua kazingua sana aseee !! Kwa hiyo katuma kama 100k hiyo marundo mengine akahamia kwa mrembo manina zake 😂😂ila atakua nazo bado ! Mungu saidia wana kikokotoo aseee
Atakua nazo , wiki mbili kweli unaweza kula bata la kumaliza 50 Mill inawezekana kweli ?Wacha akitulia atasema alitoa ngapi na huko zimebaki ngapi!
Miezi 4 tangu may 5!Atakua nazo , wiki mbili kweli unaweza kula bata la kumaliza 50 Mill inawezekana kweli ?
Alikuwa mbezi kajiteka kama roma mkatoliki!
Saivi Roma kajitekea marekaniAlikuwa mbezi kajiteka kama roma mkatoliki!
Ama kweli kwenye ulimwengu kuna dunia humo ndio kunapatikana viumbe vya kila aina!Saivi Roma kajitekea marekani
Katelekeza mke na watoto😂😂
Za chini ya kapeti rafiki yako kapatikana na msanii mmoja mkubwa tu!Ewe rafiki yangu rudi nyumbani mkeo anaumwa achana na mchepuko huo.
Miezi minne iliyopita kuna mzee aliondoka hapa kijiji cha masakata wilayani tunduru kuelekea jijini dar es salaam 'jiji la maraha.
kwenda kushughulikia miamala ya pesa zake za mafao baada ya kuhudumu serikalini kwa kipindi kirefu,
Mzee aliondoka mwezi wa tano mwaka huu kwa kumuaga bi mkubwa kuwa atarejea baada ya wiki moja.
Pia kukiwa na shabaha ya kurudi na pesa za kuwekea sawa mashamba yao,
,kweli alifika mjini akakutana na mwanawe mkubwa wa kike aliyemsaidia kurahisisha shughuli zake za kibenki.
Huyo mwanawe naye kidogo alihamdulillah anahudumu kwenye wizara moja nyeti,
Baada ya kuchukua maokoto mzee aliweza kutupa kiasi cha pesa kwa bi mkubwa baada ya hapo,
mzee hakupatikana tena si kwa simu wala salamu .
Watu walihangaika vituo vya polisi na mahospitalini ,mochwari ,baa zote na vijiwe vya kahawa ,ikawa hakuna majibu.
Cha kushtusha ni jana mzee amepatikana huko mbezi kwenye nyumba moja amefungiwa na binti mmoja umri wa mwanawe ,akiwa hana hata wasiwasi na hajui kama watu wanahangaika wala kaacha bi mkubwa huko home.
Mzee amekamata remote hana hata mashaka bi mdogo amemmwagia udambwi dambwi juu ya meza,
baada ya kumkuta hapo palizuka vurumai kubwa nguo kuchanika ili kumtoa mzee pale nyumbani kwa bi mdogo.
Huku mzee akiapa kutaka kuwaachia radhi watoto wake na bi mdogo akitaka kuwafungulia mashtaka watoto wa mzee kumletea fujo nyumbani kwake!
Angalizo :wazee wasiachwe peke yao kwenda kufanya miamala wasije angukia kwenye mikono isiyo salama!
Za matawini hazinogi mpaka uzifuatwe mjini!Aua wafungue branch huko, ukishafika huu mji basi, Kama una mafao watakula na wewe, yakiisha utasukumwa kwa mkeo.
Mkulima mmoja walaji wengi tuwakinge wazee na maharamia!Wazee wastaafu wanatia aibu sijui ni nin huwa kinawapata
Kuna mzee kastaafu kachukua chombo kipya kibichi kabisa kamzalisha mtoto kamjengea nyumba na kumfungulia duka
Mke wake alivyoona visa vinazidi mzee harudi nyumban
Kaamua kuondoka kwao na watoto nao wakafuata nyuma
Mzee kabaki na kimada wake wanatamba mtaani
Pesa zimeisha sasa ameshauza nyumba moja aliyoanza nayo maisha na mkewe , viwanja na nyumba ya familia inapigwa mnada
zikiisha kabisa najua ataanza kumtafuta mke ambaye kwasasa yupo kwa watoto wenye kazi zao patachimbika hawana hamu na baba yao
Wanaume baadhi yenu huwa mnapatwa na nin mkisha pata mafao yenu ya uzeeni au balehe huanza upya
Duh yaani nihangaike peke yangu mwisho wa siku unigande kwenye kuchukua mafao yangu,mbona wasinigande wakati wa kwenda kazini?Angalizo :wazee wasiachwe peke yao kwenda kufanya miamala wasije angukia kwenye mikono isiyo salama!
Labda edo kumwembe anaweza kuwa na hii taarifa maana ni kijiji chao!Kwa kuwa hii ni chai na kwa kuwa mzee hakusaidiwa kuzitafuta hizi hela ni zake ana haki ya kutumia atakavyo na kwa kuwa mzee ni mtu mzima mwenye akili timamu na kwa kuwa kinachowasukuma watoto kupagawa ni kudhania wangepata mgao na wameukosa na kwa kuwa hatujui maisha aliyokuwa anaishi mzee kabla hajatoka home kwenda daslam pengine alikuwa ana nyanyasika as usual kwa wanaume wakishastaafu na kwa kuwa mzee kapatikana akiwa salama haumwi na hajadhurika labda tu maokoto yamekata basi naomba nisichangie huu uzi