Aliaga anakwenda kuchukua pesa zake za mafao hakurudi!

Hapo mshua kazingua sana aseee !! Kwa hiyo katuma kama 100k hiyo marundo mengine akahamia kwa mrembo manina zake 😂😂ila atakua nazo bado ! Mungu saidia wana kikokotoo aseee
Wacha akitulia atasema alitoa ngapi na huko zimebaki ngapi!
 
Hahaaaaa, kama mazuri. Nimemkunbuka mzee mmoja nilimkutaga huko Kilolo anaitwa Upemba. Jamaa baada ya kustaafu na alikiwa mkuu qa Idara akazitumbua zote. Zilipoisha akawa amezeeka zaidi ya Baba yake mzazi na akakimbilia Mwanza kwa mkewe. Hawa wazee waandaliwe kushika pesa nyingi baada ya kustaafu.
 


Aua wafungue branch huko, ukishafika huu mji basi, Kama una mafao watakula na wewe, yakiisha utasukumwa kwa mkeo.
 
Wazee wastaafu wanatia aibu sijui ni nin huwa kinawapata
Kuna mzee kastaafu kachukua chombo kipya kibichi kabisa kamzalisha mtoto kamjengea nyumba na kumfungulia duka
Mke wake alivyoona visa vinazidi mzee harudi nyumban
Kaamua kuondoka kwao na watoto nao wakafuata nyuma
Mzee kabaki na kimada wake wanatamba mtaani
Pesa zimeisha sasa ameshauza nyumba moja aliyoanza nayo maisha na mkewe , viwanja na nyumba ya familia inapigwa mnada
zikiisha kabisa najua ataanza kumtafuta mke ambaye kwasasa yupo kwa watoto wenye kazi zao patachimbika hawana hamu na baba yao
Wanaume baadhi yenu huwa mnapatwa na nin mkisha pata mafao yenu ya uzeeni au balehe huanza upya
 
Mkulima mmoja walaji wengi tuwakinge wazee na maharamia!
 
Angalizo :wazee wasiachwe peke yao kwenda kufanya miamala wasije angukia kwenye mikono isiyo salama!
Duh yaani nihangaike peke yangu mwisho wa siku unigande kwenye kuchukua mafao yangu,mbona wasinigande wakati wa kwenda kazini?

Acha mzee ale jasho lake,ni upuuzi kumpangia mtu namna ya kutumia mali alotafuta kwa jasho lake
 
Kwa kuwa hii ni chai na kwa kuwa mzee hakusaidiwa kuzitafuta hizi hela ni zake ana haki ya kutumia atakavyo na kwa kuwa mzee ni mtu mzima mwenye akili timamu na kwa kuwa kinachowasukuma watoto kupagawa ni kudhania wangepata mgao na wameukosa na kwa kuwa hatujui maisha aliyokuwa anaishi mzee kabla hajatoka home kwenda daslam pengine alikuwa ana nyanyasika as usual kwa wanaume wakishastaafu na kwa kuwa mzee kapatikana akiwa salama haumwi na hajadhurika labda tu maokoto yamekata basi naomba nisichangie huu uzi
 
Labda edo kumwembe anaweza kuwa na hii taarifa maana ni kijiji chao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…