King Leon 1
JF-Expert Member
- Oct 25, 2019
- 245
- 342
Mwanamichezo mstaafu na mchambuzi wa michezo Amri Kiemba ameandika maoni ambayo yamenifanya niwaze na kukaa chini kutafakari juu ya kauli na maneno ya msemaji ambayo kila siku yanazidi kushangaza na kumshushia tu Professional wake.
AMRI KIEMBA ANAANDIKA:
Kuna vitu unaweza kuviangalia halafu ukatafakari kisha ukacheka ukajiuliza kwa nini Msemaji wa moja ya Klabu Kongwe nchini anababaisha?
Wote tunajua Lameck Lawi kaenda Ubelgiji kwa ajili ya kutafuta malisho bora ya maisha yake ya soka, kuna stori za kuwa alikuwa anaenda kusajiliwa moja kwa moja KAA Gent ndio hata sababu ya Coastal kurudisha pesa za Simba SC na kuna stori kuwa baada ya kufika alitakiwa kufanya majaribio na timu za vijana kitu ambacho sio kibaya.
Mchezaji kutoka katika kituo chake cha kazi kwenda nje ya nchi kwa timu nyingine kusajiliwa, kufanya majaribio hilo sio suala lake binafsi ni suala rasmi la Klabu.
Msemaji anamkosea sana Lameck Lawi kauli hizi na kama ni kweli hajafuzu majaribio unamfanya kijana ahisi kama amefeli maisha baadala ya kuongea ukwelii tu mambo hayajaenda sawa na kumpa moyo, unaamua kubabaisha, Lawi ana jambo gani binafsi Ubelgiji ambalo alisemeki? mke kajifungua? Familia au mtoto?
Ni vyema tujifunze kutoa habari za kweli au kuachana na kuzungumzia jambo kama hamko tayari kutoa taarifa za ukweli kwa hadhara.
Mwisho kufeli majaribio sio dhambi na wala haina maana huwezi kuinuka au kufika mbali.
Yaya Toure amewahi kufeli majaribio ya kujiunga na Arsenal na miaka baadae alikuja kuwa sio tu Mchezaji wa Man City bali Mchezaji anayelipwa zaidi EPL.
Ipo mifano mingi sana ila Lawi hupaswi kuvunjika moyo rudi home ujipange au tafuta timu nyingine.