Alichoandika Amri Kiemba kwa Msemaji wa Simba Ahmed Ali juu ya Lameck Lawi

Alichoandika Amri Kiemba kwa Msemaji wa Simba Ahmed Ali juu ya Lameck Lawi

Huyu Kiemba nae simuelewi, kwani Lawi wakati ana sign Simba alikuwa anafikiria kitu gani?

Kama alijua ana mpango wa kwenda Ulaya kwa majaribio kwanini hakuwaambia Simba mapema?

Kiemba hajui maana ya critical thinking, badala ya kulaumu chanzo cha tatizo, yeye analaumu matokeo ya tatizo, na wote mnaomuunga mkono kwa ujinga alioongea hamna akili pia.
Hoja ya kiemba sio kulaumu bali ni kusikitishwa kwa kauli mbaya za kumkatisha tamaa kijana tena mtanzania mwenzetu mwenye ndoto ,ilihali tunasifia wageni tu.
 
Mwanamichezo mstaafu na mchambuzi wa michezo Amri Kiemba ameandika maoni ambayo yamenifanya niwaze na kukaa chini kutafakari juu ya kauli na maneno ya msemaji ambayo kila siku yanazidi kushangaza na kumshushia tu Professional wake.

AMRI KIEMBA ANAANDIKA:

Kuna vitu unaweza kuviangalia halafu ukatafakari kisha ukacheka ukajiuliza kwa nini Msemaji wa moja ya Klabu Kongwe nchini anababaisha?

Wote tunajua Lameck Lawi kaenda Ubelgiji kwa ajili ya kutafuta malisho bora ya maisha yake ya soka, kuna stori za kuwa alikuwa anaenda kusajiliwa moja kwa moja KAA Gent ndio hata sababu ya Coastal kurudisha pesa za Simba SC na kuna stori kuwa baada ya kufika alitakiwa kufanya majaribio na timu za vijana kitu ambacho sio kibaya.

Mchezaji kutoka katika kituo chake cha kazi kwenda nje ya nchi kwa timu nyingine kusajiliwa, kufanya majaribio hilo sio suala lake binafsi ni suala rasmi la Klabu.

Msemaji anamkosea sana Lameck Lawi kauli hizi na kama ni kweli hajafuzu majaribio unamfanya kijana ahisi kama amefeli maisha baadala ya kuongea ukwelii tu mambo hayajaenda sawa na kumpa moyo, unaamua kubabaisha, Lawi ana jambo gani binafsi Ubelgiji ambalo alisemeki? mke kajifungua? Familia au mtoto?

Ni vyema tujifunze kutoa habari za kweli au kuachana na kuzungumzia jambo kama hamko tayari kutoa taarifa za ukweli kwa hadhara.

Mwisho kufeli majaribio sio dhambi na wala haina maana huwezi kuinuka au kufika mbali.

Yaya Toure amewahi kufeli majaribio ya kujiunga na Arsenal na miaka baadae alikuja kuwa sio tu Mchezaji wa Man City bali Mchezaji anayelipwa zaidi EPL.

Ipo mifano mingi sana ila Lawi hupaswi kuvunjika moyo rudi home ujipange au tafuta timu nyingine.

Ila huyu lawi kuwa 19 yrs old tumepigwa
 
Chuki tu za wabongo hakuna kingine kama mtu anamsagia kunguni kijana anaepambania maisha yake huyo sio mtu ila kwenye jamii yetu wapo wengi..
Sidhani kama amemsagia kunguni, labda kama mimi nimekuja kwa treni, siuelewi msemo huu. Angekuwa amechangia kufelisha majaribio yake, hapo sawa ingekuwa amemsagia kunguni
 
Wew mtoto mdogo huyo kiemba ana mafanikio gan kwenye mpira wa bongo land s ungesema wakina pawasa ,mogela nk
Atakuja kukujibu @gallow ila kiufupi tu Amri kiemba ni mchezaji aliezichezea club kubwa Tanzania kwa kiwango cha juu sana kama Simba,Yanga,Mtibwa,Azam,Taifa Stars na ata nje ya nchi. Kama tujuavyo mpk mtanzania kuchezea Simba na Yanga kwa wakati mmoja basi alikuwa na uwezo mkubwa sana.
 
Wew mtoto mdogo huyo kiemba ana mafanikio gan kwenye mpira wa bongo land s ungesema wakina pawasa ,mogela nk
Hapa ndo umeonesha utoto wako,kiemba alikua yanga 2005-6,simba 2013,azam,stars 2013,pawasa kacheza kipindi kifupi mno,2003 makundi klabu bingwa na simba,akakataa kwenda sweden,anaenda moro utd,akavunjika mguu,2008 anaenda cbe kusoma certificate
 
Atakuja kukujibu @gallow ila kiufupi tu Amri kiemba ni mchezaji aliezichezea club kubwa Tanzania kwa kiwango cha juu sana kama Simba,Yanga,Mtibwa,Azam,Taifa Stars na ata nje ya nchi. Kama tujuavyo mpk mtanzania kuchezea Simba na Yanga kwa wakati mmoja basi alikuwa na uwezo mkubwa sana.
Mpira huwa unachezwa hadharan ndomana amestafu mapema jiulize kwa nn pia tuje kwenye swali kiemba amefanikiwa kwenye nn lete statistics zake alikuwa anacheza kiungo
 
Hapa ndo umeonesha utoto wako,kiemba alikua yanga 2005-6,simba 2013,azam,stars 2013,pawasa kacheza kipindi kifupi mno,2003 makundi klabu bingwa na simba,akakataa kwenda sweden,anaenda moro utd,akavunjika mguu,2008 anaenda cbe kusoma certificate
Uko sahihi mkuu
 
Mpira huwa unachezwa hadharan ndomana amestafu mapema jiulize kwa nn pia tuje kwenye swali kiemba amefanikiwa kwenye nn lete statistics zake alikuwa anacheza kiungo
Kwa miaka ya zamani kulikuwa hakuna takwimu unazotaka wewe ila kwa tuliomshuhudia tunajua uwezo wake na asa akihudumu nafasi ya kiungo alikuwa mwiba sana mpaka kuweza kuimbwa na kuzichanganya club za Kariakoo kugombea saini yake.
 
Back
Top Bottom