SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Huu uzi si wa kutetea upuuzi alioufanya Ladack Chasambi katika mechi ya jana kati ya Fountain Gate vs Simba. Huu uzi nia yake kuelezea maeneo mawili ambayo Simba imekuwa na tatizo nayo kwa muda mrefu. Nasisitiza, kosa moja halihalalishi makosa mengine.
Katika mechi kati ya Simba vs Yanga ambayo kipa alikuwa Ayoub Lakred (wenye kumbukumbu mtanikumbusha ni mechi ipi), Zimbwe alimrudishia Lakred mpira wa kasi na wa juu na bahati nzuri Lakred alikuwa na control nzuri akaweza kuuclear. Kosa la Chasambi halitofautiani sana na kosa hili. Kuna mchezaji mwingine juzijuzi aliwahi kumrudishia Camara mpira wa namna hii nadhani ni Che Malone. Hakuna ubaya kumrudishia kipa mpira, swali unarudisha mpira ulio na usalama gani kwa timu yako?
Turudi kwenye tatizo la msingi la Simba:
Ukweli ni kuwa tatizo la "backpasses" limekuwa sugu pale Simba. Wengi wanadhani tunaposema "backpass" ni mpaka mpira uende kwa kipa. Hamza akiupeleka mpira kwa Zimbwe unategemea tunaenda mbele, utashangaa naye anarudisha kwa Che Malone au anapiga pasi ya pembeni kwa Kagoma. Nahisi Kocha Mgunda ndiyo alililea hili tatizo, mchezaji kama Onyango alikuwa hapigi pasi ya mbele hata siku moja, ni ama atapiga pasi ya nyuma au ya pembeni.
Robertinho akaja akajaribu kulitibu kwa "direct football", kiasi alifanikiwa ila watu wakaanza kulalamika mpira wa "butua butua" ingawa mimi sikubaliani na lebo hiyo watu walioipa.
Tusimlaumu kocha Fadlu David kwa hili tatizo. Kabla Chasambi hajajifunga, alionekana kuwahimiza wachezaji wapeleke mpira mbele ila hawakumzingatia. Kabla ya goli alilofunga Kapombe kwenye mechi ya wiki iliyopita dhidi ya Tabora, Fadlu alionekana kuwahimiza wachezaji wapeleke mpira mbele maana walionekana kuchezea mpira eneo lao bila faida. Kwa hiyo tusiseme Fadlu ndiye anayewafundisha hili.
Sielewi kwa nini baadhi ya wachezaji wa Simba wakifanyiwa pressing wanapata kitete wanaona afadhali arudishe mpira nyuma kuliko kuupoteza. Hili lilikuwa tatizo sugu hadi mchezaji anaogopa kupoteza mpira hata akiwa zone ya adui. Mchezaji anaweza kutoka na mpira kwenye kona ya adui zikapigwa pasi kurudi nyuma hadi kwa golikipa wao. Wakati mwingine wakawa wanapeana pasi za kusakiziana ingawa hili tatizo naona limepungua sana.
Jinsi ya kulitatua hili tatizo:
Niliwahi kusema ni muhimu kuwarudisha wachezaji kwenye zoezi la "angaisha bwege" au kitaalam linaitwa "rondo" au "rondos" ambalo kwa mtazamo wangu wachezaji wengi wa kitanzania hawajajua maana ya zoezi hili. Wanadhani ni kazoezi ka kujifurahisha tu wakisubiri kocha awaite waendelee na mazoezi mengine ya maana. Ukifanyiwa pressing inabidi uwe na utulivu na ubunifu wa kujua jinsi ya kucheza na wenzio, hii ndiyo faida ya kwanza ya rondos.
Angalia timu kama Man City, Real Madrid au Barcelona ilee wamekuwa na wachezaji wenye ubunifu na utulivu wa aina hii. Rondo zao zinaweza kupigwa pasi hata 30. Angalia rondo zetu hata pasi 5 ni mtihani mkubwa.
Pia ukiona kuna ulazima wa kurudisha mpira kwa golikipa, walau basi rudisha mpira wa chini kabisa unaotambaa kwenye nyasi. Hili nalo mchezaji professional anahitaji akumbushwe?