Alichokifanya Chasambi walishakifanya Zimbwe na Che Malone

Alichokifanya Chasambi walishakifanya Zimbwe na Che Malone

Achana na majanga ya "back pass" janga kubwa zaidi ni ile staili yao ya kuanza mpira nyuma kwenye boksi lao ndio iliniacha hoi siku ya mechi na Fountain Gate. Yaani washambuliaji wote watatu wa Fountain Gate wapo kwenye kona ya boksi lenu halafu mnalazimishwa lazima mpira muanzishe ndani ya boksi lenu hivyo hivyo. Hii moja kwa moja ilionyesha namna gani Simba iliidharau Fountain Gate na walichopata ilikuwa ndio haki yao. Na hili la kulazimsha kuanza mpira ndani ya boksi wakati adui amekabia juu ipo siku litasabbisha madhara kwenye mechi muhimu na mbaya zaidi mchezaji atakayesababisha ndio atalaumiwa wakati ni mfumo mbovu wa timu nzima.
 
Back
Top Bottom