Alichokifanya Gerson Msigwa, New York alipaswa akifanye Siku Zote Ikulu. Zuhura Yunus Asiwe Bubu!

Alichokifanya Gerson Msigwa, New York alipaswa akifanye Siku Zote Ikulu. Zuhura Yunus Asiwe Bubu!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
leo nilikuwa naangalia TBC Ardhio.

  1. Nikashuhudia Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akirudia kazi yake ya zamani ya utangazaji wa TV Reporting akiripotia TBC live mubashara moja kwa moja kutokea jijini New York, nchini Marekani kutuarifu maandalizi ya uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour, utakaofanyika usiku huu mida ya Saa 1:30 Kwa saa za Marekani ambapo ni saa 8:30 za usiku wa manane kwa saa za Tanzania.
  2. Msigwa ambaye sasa ndiye Msemaji Mkuu wa Serikali, amejikumbusha enzi zake za utangazaji, kwa kumhoji Msemaji Mkuu wa Serikali mstaafu Dr. Hassan Abasi ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo na Utamaduni na ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya filamu ya Royal Tour,
  3. Dr. Hassan Abbas amesema uzinduzi utahudhuriwa na wageni mashuhuri 400 akiwemo Mayor wa Jiji la New York.
  4. Kitendo cha Msemaji Mkuu wa Serikali kumhoji Msemaji Mkuu wa Serikali mstaafu ni mahojiano ya kupendeza Sana.
  5. Kiukweli kipaji cha TV Reporting na composure yake, hiki ni moja ya vipaji vikubwa sana ambavyo TBC ilivipotezea serikalini. Ndani ya TBC anayemkaribia Msigwa ni Khalid Gangana.
  6. Hongera Sana Gerson Msigwa kurudia kazi yako ya utangazaji!. Hiki ulichokifanya leo jijini New York, nchini Marekani, ndicho ulipaswa ukifanye Ikulu yetu, siku zote ilipokuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu.
  7. Kazi ya Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu, sio tuu ni kuandika Press Release, bali pia kuiripoti direct from Ikulu kwa piece to camera kama ulivyo fanya leo.
  8. Ulipaswa kuturipotia shughuli muhimu za rais ikitokea Ikulu, na kuiripoti moja kwa moja into the news.
  9. Pia ulipaswa kuitisha Press Conference na kufanya Press Briefing kwetu sisi waandishi kama walivyofanya Balozi Choks, Balozi Nkurlu na Balozi Kalaghe, na kama wafanyavyo ma Press Sec wa wenzetu Duniani.
  10. Naamini Zuhura Yunus hata kuwa Bubu, ikitokea rais ana shughuli muhimu, asiishie kutusambazia just a press release bali sasa sambazeni multi media release yenye press release, photo gallery, audio footage, TV footage, social media footage na Peace to Camera.
All and all, hongereni sana for all that you are doing, Leo sisi huku Bongo ni hakuna kulala mpaka hiyo saa 8:30 usiku wa manane.
Tunawasubiria tushuhudie.
Paskali.
Mabandiko mengine kuhusu Royal Tour Hongera Rais Samia, Kwenda US, Kuhutubia UN, Safari ya Kuzindua Filamu Yako ya Royal Tour, Tunaomba Tukusindikize, Dreamliner Yetu Itue New York

na Je, Uzinduzi Royal Tour ungekuwa na maana kama Rais Samia angetua kwa Dreamliner & ATC kuzindua Direct Flights from DAR-JFK-DAR/JRO-JFK-JRO?

na Hongera Rais Samia Kuzindua Filamu ya Royal Tour Marekani, Ingenoga Zaidi Kama Mama Angetua Marekani na Dreamliner Full of Wabongo!
 
Waraka wa Press release wanaweza kukanusha na kuandika FAKE FAKE...
Sauti na sura zao hawawezi.
Labda siasa zisiingilie kati taaluma zao!!😂😂😂
 
Kwa hiyo unasema zuhura Yunisi ni mfanyakazi hewa na hajui hii kazi
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
 
Vya kwetu vyazinduliwa kwao ilitakiwa izinduliwe juu ya mrima kilimanjaro
 
Back
Top Bottom