Alichokifanya Manara ndicho alichofanya Dr Willbroad Slaa 2015

Riz king

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2018
Posts
276
Reaction score
549
Hizi tabia za kitanzania na za kihuni kuwa huwezi ondoka kwenye taasisi kimya bila kusema mabaya ni malezi ya ajabu sana. Mimi ni mwana yanga kindakindaki lakini alchofanya manara na alichofanya Dr Slaa wakati ule wa 2015 vinafanana.

Tujifunze kuwa wakimya maana kama ni ubaya wa kitu huja kujionyesha wenyewe sio mpaka mtu atoke kutumia nguvu kuusema wakati na yeye alikuwa ndani ya taasisi. Wakati wa mabadiliko aliyapamba tukamwamini hii leo anakuwa kama mwanamke. Alimsema senzo vibaya sana, lakini hii leo anamkumbuka kwa kumlindia kibarua Simba. Tujifunze kutowaendekeza watu katika maisha yetu.

Na ntakuwa mwana Yanga wa kwanza kupinga huu ujinga wa Manara.
 
Manara hajagombana na Simba! Mapenzi yake kwa simba yako palepale ila issue za maslahi zimemgombanisha na mabos wake.
 
Mimi nimefurahia sana tukio la huyo Hajji Manara kuwachana live hao waajiri wake! Huyo jamaa hana tofauti na Jini! Walimlea wakati ule anaitukana na kuikejeli Yanga kama timu, wachezaji wake, viongozi na mashabiki!

Leo hii amewageuka walio mvimbisha kichwa!! Narudia tena kusema, safi sana!! Bravo!!!
 
Hebu kwanza Kuna sijaelewa vizuri: Anasema Mo kaweka bilion 20 na vilevile anaidai Simba ssc bilion 21? Ufafanuzi tafadhari
 
'Hii tabia ya kitanzania...' wala sio shida ya watanzania, hii tabia ipo mahali pengi tu duniani,tusijikandie sana.
 
Namkubali sana manara, anajua maana ya kuwa msemaji wa taasisi, naamini atafanikiwa popote aendako
 
Mo ni tapeli. CAG akakague hesabu za simba. Yaliyomkuta manara ni mambo ya wahindi. Wahindi wanapenda kudhurumu ngozi nyeusi.
 
Manara ni mshenzi tu hana mapenzi yoyote na Simba.

Ni mtu mbinafsi anayejali maslahi yake tu na akiyapata anafanya unafiki wa kujidai anaioenda Simba.

Angekuwa anaipenda Simba asingeanzisha timbwili siku chache kabla ya derby.Na hata sasa anaiombea mabaya Simba
Manara hajagombana na Simba! Mapenzi yake kwa simba yako palepale ila issue za maslahi zimemgombanisha na mabos wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…