Alichokitaka Manara kwa TFF amefanikiwa

Yanga inaendeshwa kihuni sana.viongozi wahuni,wanawaburuza mashabiki . mashabiki wenyewe akili hawana.wao wanaona wanaonewa tu.manara anawashika mapembe ndo wanazidi kuchanganyikiwa.
Hahahaaa
 
-utasikia wakati nafanya kazi TFF, kila akielezea jambo lazima akazie kuwa alifny kazi TFF
-baada ya haji kumtukana rais wa TFF eti akampigia rais kumpa pole loh!

Kama nyie mnavyotafuta ugali na haji nae anatafuta ugali vilevile, achen kutumika kuwadiscredit wakosoaji wa karia maana nyie mmeshazibwa midomo kwa zile nafasi za kamati mbalimbali mlizopewa au Mnazoziitolea macho,
 
Yanga ni kubwa kuliko TFF, YANGA ni nchi ndani ya nchi, Yanga ni kama mamlaka ya nchi .

Kisinda atacheza watake wasitake ukibisha utaona ni jambo la muda tu.
 
Sote tuliudhika na Mwakinyo kupoteza pambano afu ukizingatia kwa sababu nyepesi tu, ila hatua aliyofikia Manara ni extreme.

Ni kawaida yake kuwaona critics kama watu wenye chuki lakini leo hii kaja kufanya kile kile ambacho yeye amekuwa akichukia akifanyiwa yeye.

Tena kafanya kwa kiwango kisicho cha uungwana na sio professionalism
 
Yanga ni kubwa kuliko TFF, YANGA ni nchi ndani ya nchi, Yanga ni kama mamlaka ya nchi .

Kisinda atacheza watake wasitake ukibisha utaona ni jambo la muda tu.
Tii sheria bila shuruti huo ukubwa mnaojipa sio kitu mbele ya sheria

Ukubwa wa bila kutambua sheria na kuziheshimu huo ni ukubwa jinga.

Mi nataka niwaone Yanga wakitetea hoja zao kwa kutaja vifungu vya sheria ambavyo vimekiukwa na TFF, sio kusema mnaonewa kwasababu tu hupendi kuona timu yako inapata dhoruba hata kama imekiuka sheria.

Tafuteni wasomi wawe viongozi, wale wazee umri umeenda sana ni ngumu kuwategemea kwenye moments kama hizi.
 
Hawa vitoga wamezoea kushikiwa akili na watu wachache waliowapa dhamana kuwa muda wote wanayoyasema huwa ni kweli.

Huu usajili wa Kisinda kama waliweka kimtego ili tu kutafuta justification ionekane TFF inachuki na Yanga basi wamefeli sana.

Na mwisho wa siku conspiracy yao inakuja kumgharimu mchezaji husika.

Huyu Kisinda swala la kucheza ndio ajira yake, hata kama Yanga watakuwa willing kumpa mshahara pasipo kushiriki michuano kusubiria dirisha dogo bado haitasaidia.

Mshahara sio kitu cha kumfanya mchezaji azidi kufurahia, mchezaji lengo lake siku zote ni kujitangaza kimataifa, na ili ajitangaze lazima acheze aoneshe ubora wake uwavutie watu wengine.

Sasa kama watazidi kumuweka kapuni mpaka wasubirie dirisha dogo basi huo utakuwa ni ukatiri na Kisinda kama akiamua kufika mbali anaweza akawapeleka Mahakamani uongozi wa Yanga wakapata hasara kubwa ambayo hawakuitegemea.
 
SIKU MANARA ALIPOSEMA NIMEHAMA SIMBA KUJA YANGA NDIO NILIMUONA INJINIA WA MCHONGO HERSI SAID NI KILAZA KULIKO MAELEZO

HERSI SAID NA GSM WANAAMINI BILA MANARA HAMNA YANGA WAKATI YANGA IMEANZISHWA 1935 KABLA YA VITA YA PILI YA DUNIA!
 
Sawa mkuu
 
Kwa wapenzi na wadau wote wa soka habari za wakati huu nawasalimu kwa jina la tozo na makato yaendelee.[emoji23]
Mkuu unanisalimia au unajibu salam mkuu
 
Yanga tatizo wanalalamika hata vitu ambavyo ni kweli wamekosea wanafanya maksudi ili wakipewa adhabu waseme karia ni mbaya
 
Yanga ni kubwa kuliko TFF, YANGA ni nchi ndani ya nchi, Yanga ni kama mamlaka ya nchi .

Kisinda atacheza watake wasitake ukibisha utaona ni jambo la muda tu.
Acheze au asicheze karia hana chochote anachopata anachotaka mfuate sheria majina ya yanga princess yametumwa mda ulishapita ila wamesajili hvyo hvyo kuepuka lawama.
 
Yanga ni kubwa kuliko TFF, YANGA ni nchi ndani ya nchi, Yanga ni kama mamlaka ya nchi .

Kisinda atacheza watake wasitake ukibisha utaona ni jambo la muda tu.
Ni kubwa kuliko familia yako sio Tff
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…