Alichokitaka Manara kwa TFF amefanikiwa

Alichokitaka Manara kwa TFF amefanikiwa

Elimu
Elimu
Elimu
IMG-20220905-WA0000.jpg
 
Yanga inaendeshwa kihuni sana.viongozi wahuni,wanawaburuza mashabiki . mashabiki wenyewe akili hawana.wao wanaona wanaonewa tu.manara anawashika mapembe ndo wanazidi kuchanganyikiwa.
Hahahaaa
 
-utasikia wakati nafanya kazi TFF, kila akielezea jambo lazima akazie kuwa alifny kazi TFF
-baada ya haji kumtukana rais wa TFF eti akampigia rais kumpa pole loh!

Kama nyie mnavyotafuta ugali na haji nae anatafuta ugali vilevile, achen kutumika kuwadiscredit wakosoaji wa karia maana nyie mmeshazibwa midomo kwa zile nafasi za kamati mbalimbali mlizopewa au Mnazoziitolea macho,
 
Yanga ni kubwa kuliko TFF, YANGA ni nchi ndani ya nchi, Yanga ni kama mamlaka ya nchi .

Kisinda atacheza watake wasitake ukibisha utaona ni jambo la muda tu.
 
Kwa wake mambwiga mnaomtetea Haji oneni uchokozi huu kwa Mwakinyo,akijibiwa sawa na wazimu wake mnasema anaonewa kwa vile ni zeruzeru. Jee Haji anayokinga ya kutukana watu bila kujibiwa kwa huo uzeruzeru wake? Matusi yote kwa Mwakinyo ni kwa vile tu Mwakinyo ni mshabiki wa Simba.
Sote tuliudhika na Mwakinyo kupoteza pambano afu ukizingatia kwa sababu nyepesi tu, ila hatua aliyofikia Manara ni extreme.

Ni kawaida yake kuwaona critics kama watu wenye chuki lakini leo hii kaja kufanya kile kile ambacho yeye amekuwa akichukia akifanyiwa yeye.

Tena kafanya kwa kiwango kisicho cha uungwana na sio professionalism
 
Yanga ni kubwa kuliko TFF, YANGA ni nchi ndani ya nchi, Yanga ni kama mamlaka ya nchi .

Kisinda atacheza watake wasitake ukibisha utaona ni jambo la muda tu.
Tii sheria bila shuruti huo ukubwa mnaojipa sio kitu mbele ya sheria

Ukubwa wa bila kutambua sheria na kuziheshimu huo ni ukubwa jinga.

Mi nataka niwaone Yanga wakitetea hoja zao kwa kutaja vifungu vya sheria ambavyo vimekiukwa na TFF, sio kusema mnaonewa kwasababu tu hupendi kuona timu yako inapata dhoruba hata kama imekiuka sheria.

Tafuteni wasomi wawe viongozi, wale wazee umri umeenda sana ni ngumu kuwategemea kwenye moments kama hizi.
 
Hawa vitoga wamezoea kushikiwa akili na watu wachache waliowapa dhamana kuwa muda wote wanayoyasema huwa ni kweli.

Huu usajili wa Kisinda kama waliweka kimtego ili tu kutafuta justification ionekane TFF inachuki na Yanga basi wamefeli sana.

Na mwisho wa siku conspiracy yao inakuja kumgharimu mchezaji husika.

Huyu Kisinda swala la kucheza ndio ajira yake, hata kama Yanga watakuwa willing kumpa mshahara pasipo kushiriki michuano kusubiria dirisha dogo bado haitasaidia.

Mshahara sio kitu cha kumfanya mchezaji azidi kufurahia, mchezaji lengo lake siku zote ni kujitangaza kimataifa, na ili ajitangaze lazima acheze aoneshe ubora wake uwavutie watu wengine.

Sasa kama watazidi kumuweka kapuni mpaka wasubirie dirisha dogo basi huo utakuwa ni ukatiri na Kisinda kama akiamua kufika mbali anaweza akawapeleka Mahakamani uongozi wa Yanga wakapata hasara kubwa ambayo hawakuitegemea.
 
SIKU MANARA ALIPOSEMA NIMEHAMA SIMBA KUJA YANGA NDIO NILIMUONA INJINIA WA MCHONGO HERSI SAID NI KILAZA KULIKO MAELEZO

HERSI SAID NA GSM WANAAMINI BILA MANARA HAMNA YANGA WAKATI YANGA IMEANZISHWA 1935 KABLA YA VITA YA PILI YA DUNIA!
 
Kwa wapenzi na wadau wote wa soka habari za wakati huu nawasalimu kwa jina la tozo na makato yaendelee.

twende kwenye mada:–

Manara ni mtu mmoja mbinafsi sana anayeendekeza chuki na visasi kwa mashabiki wa team pinzani au kwa viongozi ambao yeye ana tofauti nao ili aonekane yeye ndo yupo sahihi au anaonewa hata kipindi yupo simba aliwapiga marufuku mashabiki wa yanga wasiingie taifa kwenye mechi za simba ila leo wamesahau na wanamuunga mkono kila kitu anachosema.

Baada ya manara kupewa adhabu na TFF alitaka kuwaaminisha watu kwamba amepewa adhabu ili kuidhoofisha yanga unajiuliza yeye sio mchezaji wala hayuko katika nafasi za uongozi wa juu sasa kwa nini aseme yanga inataka kudhoofishwa kupitia yeye wakati kipindi yupo simba wananchi walikuwa wanafanya mambo yao wenyewe bila yeye.

Amefanikiwa kueneza chuki kwa mashabiki wa yanga ili waichukue TFF na kweli amefanikiwa kwenye hilo hata akipewa adhabu yeye binafsi ataihusisha na yanga hata kama kweli kuna makosa na kila mtu anaona amefanya kama alivyoenda kwenye yanga day wakati anajua kabisa ana adhabu sijui kiburi anatoa wapi yule mtu inawezekana ikawa kweli TFF na yanga wana tofauti ila anachokifanya yeye ni kuongeza tatizo ili TFF ionekane ina makosa kitu ambacho sio sahihi.

Juzi kwenye dirisha la usajili wakati linakaribia kufungwa team ya wanawake ya yanga princess ilikuwa miongoni mwa team ambazo zilikuwa hazija sajili majina ya wachezaji wao na wakakumbushwa kufanya hvyo hapo walikuwa wametega likitokea la kutokea wajifiche kwenye kivuli cha kuonewa na TFF kwa hilo manara amefanikiwa.

Wachezaji wa yanga wakigeni wanaonekana kwa idadi wamezidi 12 je ni kweli walipeleka jina mapema la mchezaji wanaetaka kumuacha na kumuongeza au hawakuwa na uhakiki wa dili kukamilika na walipogundua wameshindwa wakaamua wajifiche kwenye kivuli cha kuonewa na TFF unajiuliza kwani wao TFF wanafaidika na nini kisinda akisajiliwa au asiposajiliwa kwenye system tatizo la mashabiki wa yanga wanabeba taarifa kama ilivyo kutoka kwa manara iwe ya propaganda au ya kweli kwa hilo amefanikiwa.

Juzi wamepewa adhabu na TFF ila badala waangalie tatizo la adhabu waliyopewa wakajificha kwenye rafu ya inonga na kuonewa na TFF kitu ambacho manara ndo anakitaka na ndo kinampa furaha na kwa hilo kweli wamefanikiwa kuwagombanisha na TFF.

Haya mnamuacha nani kati ya wachezaji 13 mnaotaka tifua tifua wawasajili wote kwenye mfumo ili muweze kuwatimia.

NB: Manara alifungiwa kujihusisha na mpira maisha ila karia ndo alimtoa kwenye kifungo hicho kwa hyo kufungiwa hajaanza kufungiwa akiwa yanga ieleweke hvyo ili twende sawa.
Sawa mkuu
 
Kwa wapenzi na wadau wote wa soka habari za wakati huu nawasalimu kwa jina la tozo na makato yaendelee.[emoji23]
Mkuu unanisalimia au unajibu salam mkuu
 
-utasikia wakati nafanya kazi TFF, kila akielezea jambo lazima akazie kuwa alifny kazi TFF
-baada ya haji kumtukana rais wa TFF eti akampigia rais kumpa pole loh!

Kama nyie mnavyotafuta ugali na haji nae anatafuta ugali vilevile, achen kutumika kuwadiscredit wakosoaji wa karia maana nyie mmeshazibwa midomo kwa zile nafasi za kamati mbalimbali mlizopewa au Mnazoziitolea macho,
Yanga tatizo wanalalamika hata vitu ambavyo ni kweli wamekosea wanafanya maksudi ili wakipewa adhabu waseme karia ni mbaya
 
Yanga ni kubwa kuliko TFF, YANGA ni nchi ndani ya nchi, Yanga ni kama mamlaka ya nchi .

Kisinda atacheza watake wasitake ukibisha utaona ni jambo la muda tu.
Acheze au asicheze karia hana chochote anachopata anachotaka mfuate sheria majina ya yanga princess yametumwa mda ulishapita ila wamesajili hvyo hvyo kuepuka lawama.
 
Yanga ni kubwa kuliko TFF, YANGA ni nchi ndani ya nchi, Yanga ni kama mamlaka ya nchi .

Kisinda atacheza watake wasitake ukibisha utaona ni jambo la muda tu.
Ni kubwa kuliko familia yako sio Tff
 
Back
Top Bottom