Alichonifanyia Trafiki huyu sitasahau

Alichonifanyia Trafiki huyu sitasahau

Japhet Karibu

Member
Joined
Feb 27, 2020
Posts
79
Reaction score
129
Jana natoka zangu nyumbani nikiwa nimefunga mkanda wangu wa gari kama kawaida kwa ajili ya usalama wangu barabarani. Nimeendesha gari mpaka eneo la buzuruga stand iliyopo Nyakato Mwanza nikamuacha mwenzangu niliyekuwa naye ndani ya gari yangu.

Nikaondoka kupitia njia ya kutoka Buzuruga Stand kuelekea Kilimahewa ile nafika maeneo ya Sabato Darajani nikasimamishwa na na trafiki jina ninalo. Kisha kasogea kwenye gari yangu akaniomba leseni yangu na kuniuliza unajua kosa lako nikasema hapana.

Akasema kosa lako hujafunga mkanda wa gari na hapo toka nyumbani kwangu sijafungua mkanda kutoka kifuani kwangu nikamwambia askari mbona toka nyumbani kwangu sijafungua mkanda akasema ngoja nikuoneshe kuwa nina mamlaka kiukweli aliniandikia faini ya elfu thelathini kwa uonevu mkubwa lakini pia iliniuma sana nikajiuliza kumbe hata trafiki anaweza kukubambikia kosa niliumia sana mpaka leo sijasahau.

Na hapa nilipo nina deni la elfu thelathini la uonevu ninalotakiwa kulipa ndani ya wiki. Ndugu matrafiki hata kama mnapata bonasi kwenye hizo faini mnazotupiga kwa kutubambikia makosa Kwaresma hii mbadilike. Ushauri wenu faini sijailipa bado inaniuma sana.
 
Shida ni kwamba wewe ni msemaji upande wa kwanza.tungemsikia na traffic nayeye.
 
Basi wewe boya...Mimi ningemfunga na mkanda wa shingo mamaaee.30,000 bora niwanunulie wanangu mguu wa Mbuzi

Sent using Jamii Forums mobile app

Unajibu tu hapo leseni wana chukua anakuandikia tu faini tena hata bila wewe kujua ukija siku nyingine unakuta imeshakuwa mara mbili. Ni uonevu na wizi tu. Pale Tabata alinikamata mmoja akakagua leseni una simu hapo nikamwambia yes basi mwezi mmoja baadae nikasimamishwa Magomeni kagera na wale wa vikamera DENI elfu 60 mahali TABATA nikachoka. Wizi tupu
 
Hapo tabata walinidaka sijatembea na kadi ya gari, yule fala alinikomalia akaniandikia 30
Unajibu tu hapo leseni wana chukua anakuandikia tu faini tena hata bila wewe kujua ukija siku nyingine unakuta imeshakuwa mara mbili. Ni uonevu na wizi tu. Pale Tabata alinikamata mmoja akakagua leseni una simu hapo nikamwambia yes basi mwezi mmoja baadae nikasimamishwa Magomeni kagera na wale wa vikamera DENI elfu 60 mahali TABATA nikachoka. Wizi tupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jamaa anafanya kazi na huyo trafiki kaniambia ni kweli walikamata mtu mwenye kosa kama lako! Lakini Askari huyo anadai kwamba ulipigwa mkono ukiwa hujafunga mkanda, ulipoona hivyo ukawahi kufunga mkanda wakati ukipaki pembeni;

.Askari alikuomba leseni, na akakuuliza maswali na kuandika kwenye kitabu cha kukubalikosa au KUKATAA KOSA ;
Na wewe ulichagua kukubali kosa ndiyo maana ULIANDIKIWA!

Hivyo kalipe tu mjomba; Nchi haijengwi kwa mawe!
 
Back
Top Bottom