Entim
JF-Expert Member
- Jun 7, 2013
- 4,025
- 2,261
Post jina lake humu tuwapatie PCCB Makao Makuu watamfuatilia.
Cc; RPC Mwanza
Sent using Jamii Forums mobile app
Cc; RPC Mwanza
Jana natoka zangu nyumbani nikiwa nimefunga mkanda wangu wa gari kama kawaida kwa ajili ya usalama wangu barabarani. Nimeendesha gari mpaka eneo la buzuruga stand iliyopo Nyakato Mwanza nikamuacha mwenzangu niliyekuwa naye ndani ya gari yangu.
Nikaondoka kupitia njia ya kutoka Buzuruga Stand kuelekea Kilimahewa ile nafika maeneo ya Sabato Darajani nikasimamishwa na na trafiki jina ninalo. Kisha kasogea kwenye gari yangu akaniomba leseni yangu na kuniuliza unajua kosa lako nikasema hapana.
Akasema kosa lako hujafunga mkanda wa gari na hapo toka nyumbani kwangu sijafungua mkanda kutoka kifuani kwangu nikamwambia askari mbona toka nyumbani kwangu sijafungua mkanda akasema ngoja nikuoneshe kuwa nina mamlaka kiukweli aliniandikia faini ya elfu thelathini kwa uonevu mkubwa lakini pia iliniuma sana nikajiuliza kumbe hata trafiki anaweza kukubambikia kosa niliumia sana mpaka leo sijasahau.
Na hapa nilipo nina deni la elfu thelathini la uonevu ninalotakiwa kulipa ndani ya wiki. Ndugu matrafiki hata kama mnapata bonasi kwenye hizo faini mnazotupiga kwa kutubambikia makosa Kwaresma hii mbadilike. Ushauri wenu faini sijailipa bado inaniuma sana.
Sent using Jamii Forums mobile app