Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Habari,
Leo asubuhi nilipokea ujumbe kwa namba ngeni ukisema "Mbona siku zinakwenda upo kimya" Mwisho kajitambulisha kuwa ni mwenye nyumba. Nikajua tu ni tapeli wa mtandaoni anajaribu bahati huenda akatumiwa pesa na mmoja wa wapangaji wanaodaiwa na wenye nyumba.
Nikampigia akapokea simu kwa ujasiri na kwa sauti zile za matapeli wa kimtandao. Maana mara nyingi tu wanapiga kwenye simu yangu au ya wife kwa issue mbalimbali. Wife amewahi kunusurika kutapeliwa baada tu ya kupata pesa za mirathi nikamsanua akakwepa mtego.
Huyu tapeli wa leo nikamwambia kuwa kila siku matapeli wenzako wanashikwa, tena wengine walijipanga na kuwa makini kama wewe au zaidi ya wewe. Hivyo ipo siku utakamatwa na utayakumbuka maneno yangu ukiwa selo.
Akanijibu hivi "Nisikilize ndugu, kila siku tunashikwa lakini tunatoa pesa tunaachiwa tunaendelea kutapeli". Akaendelea kuniambia kuwa hivi brother tangu uanze kuona tunashikwa na sometimes kutangazwa kwenye vyombo vya habari umewahi kusikia kuwa tumefungwa? Tuliishia hapo. Aliniacha na tafakuri kubwa.
Ma RPC wanapotangaza kwa mbwembwe pindi wakiwapata hawa matapeli, kesi zao hazifiki Mahakamani au zinafika lakini zinaishia huko mahakamani? Je, hii nchi hakuna chombo kinachofuatilia mwenendo wa chombo kingine? Je, Serikali imeridhia kuwa pesa iwe jawabu la mambo yote hata ya uuaji, ujambazi, utapeli na ubakaji?