Alichonijibu huyu tapeli wa mtandao kimenifanya nitafakari mno juu ya Taifa langu Tanzania

Alichonijibu huyu tapeli wa mtandao kimenifanya nitafakari mno juu ya Taifa langu Tanzania

Siku moja afisa wa PCCB Lindi aliniambia kuwa ashatoa rushwa kwa afisa wa HQ apate uhamisho. Kweli akahamishiwa Dar
Yaani hata wakiwa wanchunguza kesi ya rushwa wanomba rushwa tena.Ndiyo maana watoa taarifa wameamua kukaa kimya. sababu ukitaarifu watachukua rushwa halafu watakutaja kwa uliyemreport
 
Juzi tu nilipigiwa na tapeli mmoja na akajitambulisha kuwa ni mtoa huduma kutota Vodacom. Na mm nikavutiwa kuona jinsi gani anaongea kwa ujasiri kiasi kile. Ikabidi nimpe muda ajieleze tu vizuri na nikamuuliza lengo lake hadi kunipigia simu ni lipi?(namba yake ilikuwa ya tigo ...47).

Tapeli si akaanza kuniambia nimesitishiwa huduma ya M-PESA kwenye line yangu, na mimi nikamuuliza kwahvyo unanisaidiaje?

TAPELI: ili kufunguwa line yako iweze kuruhisiwa unatakiwa kupiga*33*0000# na kuiruhusu alafu unisomee ujumbe nikupe muongozo....

alipo niambia hivyo tu!! nikawa nimezifahamu hizo code na nikajuwa hapa ni kuifungia line isiweze kufanya mawasiliano ya aina yoyote. Na mm nikamwambia tayari na nikamsomea ujumbe kama alivyo tegemea. Baada ya hapo nikamuuliza, "Hivi una uhakika na unachokitafta?". Jamaa likaingia mitini kama utani nikaandika ujumbe mfupi na nikamtumia kupitia ile namba aliyokuwa amenipigia.

Ilikuwa ni asubuhi, ile jioni tapeli akanipigia simu. Tuliongea mazungumzo ya kawaida tu ila lengo alilokuja nalo nikutaka ushirikiano wangu tupige kazi wote..🤣🤣
Ndio nikagunduwa kumbe hawa matapeli ni njaa ndio inawasukuma kufanya huu ujinga ila wengi wao hukurupuka bila kukaa chini na kuja na plani.(kwa mfumo huu serikali inatakiwa kuwachukulia hatuwa bila huruma).
 
Habari,
Leo asubuhi nilipokea ujumbe kwa namba ngeni ukisema "Mbona siku zinakwenda upo kimya" Mwisho kajitambulisha kuwa ni mwenye nyumba. Nikajua tu ni tapeli wa mtandaoni anajaribu bahati huenda akatumiwa pesa na mmoja wa wapangaji wanaodaiwa na wenye nyumba.

Nikampigia akapokea simu kwa ujasiri na kwa sauti zile za matapeli wa kimtandao. Maana mara nyingi tu wanapiga kwenye simu yangu au ya wife kwa issue mbalimbali. Wife amewahi kunusurika kutapeliwa baada tu ya kupata pesa za mirathi nikamsanua akakwepa mtego.

Huyu tapeli wa leo nikamwambia kuwa kila siku matapeli wenzako wanashikwa, tena wengine walijipanga na kuwa makini kama wewe au zaidi ya wewe. Hivyo ipo siku utakamatwa na utayakumbuka maneno yangu ukiwa selo.

Akanijibu hivi "Nisikilize ndugu, kila siku tunashikwa lakini tunatoa pesa tunaachiwa tunaendelea kutapeli". Akaendelea kuniambia kuwa hivi brother tangu uanze kuona tunashikwa na sometimes kutangazwa kwenye vyombo vya habari umewahi kusikia kuwa tumefungwa? Tuliishia hapo. Aliniacha na tafakuri kubwa.

Ma RPC wanapotangaza kwa mbwembwe pindi wakiwapata hawa matapeli, kesi zao hazifiki Mahakamani au zinafika lakini zinaishia huko mahakamani? Je, hii nchi hakuna chombo kinachofuatilia mwenendo wa chombo kingine? Je, Serikali imeridhia kuwa pesa iwe jawabu la mambo yote hata ya uuaji, ujambazi, utapeli na ubakaji?
...Na kweli ! Kesi zao Huwa hatuzikii...!!
 
Back
Top Bottom