Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Viongozi wa upinzani nchini wamekuwa wanafiki sana. DC Longido amewaeleza madiwani kwamba kama siyo serikali wasingepita bila kupingwa. Huu ndio ukweli na hakuna asiyejua. Lakini maneno haya wanataka kuyachukulia kama vile DC ana kiburi na ubabe wakati ukweli haya ndiyo maneno wamekuwa wanayasema jukwaani kila siku.
DC amewaeleza madiwani kwamba uchaguzi ujao hautakuwa wakupita bila kupingwa na amewataka wachape kazi.
Amesema wao kama chama tawala wamepita kila kijiji kukusanya taarifa za hali ilivyo; je vyama vya upinzani wanashindwa nini kupita kila kijiji kama wenzao.
Siasa siyo mchezo wakioneana huruma bali ni mchezo wakushawishi. Lisu hata siku moja hajawahi kupongeza tumbua tambua inayofanywa kwa sababu anafahamu wanaotumbuliwa ni wana mkakati wa CCM na bado wataendelea kutumika.
Kutumbuliwa kwa nape na makamba kumewanufaishaje chadema na wapinzani? Tuache siasa za kushabikia michezo ya CCM turudi kuandaa wapiga kura.
Maneno ya DC yamewahi kuzungumzwa na watu wengi na CCM ikiona kelele zimekuwa nyingi wanajipangia kazi nyingine.....wakiwapangia wati wao kazi nyingine wapinzani mnashangilia katumbuliwa.
Acheni kulaghaiwa na agenda za ccm, hii kauli ya DC imekuja kuzima mjadala wa Katibu Mkuu kukwepa mdahalo.
Pia soma:Kuelekea 2025 - Mdahalo wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa: Nchimbi kaingia mitini, wengine wagoma kushiriki!