Alichosema Manara kuelekea mechi Ud Songo

marcoveratti

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
1,019
Reaction score
1,824
"Kwetu mashabiki sio mchezaji wa 12, ni mchezaji wa kila nafasi uwanjani. Tunashinda lakini mashabiki wanachangia sana"- Haji Manara. #NguvuMoja

"Simba ndio timu ambayo imeongoza msimu uliopita kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kujaza mashabiki uwanjani. Tunataka tuliendeleze hilo mwaka huu."- Haji Manara. #NguvuMoja

"Na bahati nzuri mchezo wetu wa Ligi ya Mabingwa umepangwa siku nzuri. Utakuwa Jumapili saa 10 jioni."- Haji Manara. #NguvuMoja

"Tunataka mashabiki mshabikie mwanzo mwisho. Tusisubiri mpaka Shiboub apige mtu chenga, mashabiki tunaenda uwanjani kushabikia."- Haji Manara. #NguvuMoja

"UD Songo sio timu ya kupeza. Tumeona mechi yao wamecheza vizuri. Nawaomba mashabiki wa Simba siku hiyo tujitokeze kwa wingi."- Haji Manara. #NguvuMoja

"Kwa mashabiki wa Simba hii ni Champions League, kazi yetu mashabiki ni kushabikia, twendeni."- Haji Manara. #NguvuMoja

"Matumaini yangu tutawatoa UD Songo. Kwa maandalizi yetu, mipango na mapenzi ya Mungu tutashinda."- Haji Manara. #NguvuMoja

VIINGILIO VYA JUMAPILI TAIFA
5,000/=, 15,000/=, 30,000/=
Platinum 100,000/=
Platinum plus 150,000/=
UD Songo watawasili Ijumaa.

SIMBA NGUVU 1[emoji91][emoji91][emoji91][emoji1377][emoji1377]
WE ARE SIMBAAAAA[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji382][emoji382]

Usipitwe na chochote kuhusu Simba sc
[emoji116][emoji116][emoji116]simba [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…