Aliecheza kama yesu aomba watu waache kumuabudu "Mimi sio Yesu"

Aliecheza kama yesu aomba watu waache kumuabudu "Mimi sio Yesu"

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Brian Deacon, mwigizaji mashuhuri wa nchini Uingereza aliyetokea katika familia ya kawaida ya fundi magari na muuguzi mjini Oxford, amejikuta katikati ya mjadala mzito wa kiimani duniani kote. Akiwa kaka mkubwa wa mwigizaji Eric Deacon, Brian alipata umaarufu mkubwa mwaka 1979 baada ya kuigiza kama Yesu Kristo kwenye filamu maarufu ya "Jesus".

Hata hivyo, kutokana na umaarufu wa filamu hiyo, sura yake ilianza kutumiwa vibaya kama taswira halisi ya kidini, hususan barani Afrika ambako watu wengi wamekuwa wakimfahamu na hata kumwabudu kupitia picha zake.

Kutokana na hali hiyo, ametoa wito kwa jamii na waumini kote duniani kuondoa picha za mwigizaji huyo zilizotundikwa kuta za makanisa, sebuleni, na vyumbani.

Ukweli uliopo ni kwamba Brian Deacon ni binadamu na mwigizaji wa taaluma tu, na picha zote zinazosambazwa si taswira halisi ya Yesu wa historia, bali ni picha zilizopigwa wakati wa uandaaji wa filamu hiyo ya mwaka 1979. Hatua ya kuondoa picha hizo inalenga kusaidia waumini kutenganisha kati ya sanaa ya drama na msingi wa imani zao za kidini.
1789646449774.png

1789646483724.png
 
Back
Top Bottom