Watanzania wanakabiliwa na ujinga mwisngi na generalisation syndrome, hawana muda wa kutafta facts, wao wanaenda na upepo tu wowote hasa wa uzushi ni rahisi sana kuwakamata.
Utasikia wanawake wa kihaya malaya, unajiuliza ina maana wanawake wote wa kihaya ni malaya hakuna alieolewa wote wanauza uchi barabarani?
Utasikia Wanawake wa machame wanaua wanaume unajiuliza kwa hiyo machame yote hakuna wanaume wote wameuwawa?
Utasikia wakurya wanapiga wanawake, unajiuliza wanawake wote wanaopigwa kina uchebe alikua anamfumua Shilole, Chris brown alimdunda Rihana wote ni wakurya?
Ukiwasikiliza watanzania wengi hutafanya lolote, maana wana negativety kwa kila kabila.
Hii tabia ya kuhusisha tabia ya mtu na watu wote wa kabila lake ni ujinga wa hali ya juu sana. Mwalimu alipambana na ujinga lakini amekufa ameacha ujinga ndio imeshamiri.