Alifungwa jela miaka 30 akituhumiwa kuua, lakini alipotoka gerezani akamuona aliyedaiwa kumuua

Siyo Movies ndg hii Marekani imetokea Sana cha msingi jibu swali hapo Kama itatokea hiyo how could you solve it in accordance to ur proffesional
 
Swali; Ameshafanya au anataka kwenda kufanya hayo mauaji? Afanye hivi; Kwanza afanye juu chini kuweza kuthibitisha huyo jamaa ndiye kweli aliye tangazwa kuwa alimuua. Atafute rekodi za kimahakama na hukumu yake iliyotolewa kuwa afungwe kwa kumuua Mr. X. Akiisha kuhakikisha kavipata hivyo, basi aende akamkamate vizuri mtu wake, amuue taratiibu kabisa ahakikishe kafwa fwiiii. Ajiendee nyumbani baada ya kumwachia ujumbe kuwa; Nimekurudisha ulikotoroka kwani nilishapewa adhabu ya kukutuma huko. Nimekukuta kumbe umetoroka huko sasa nimekurudisha huko kuzimu kwenyu.
Auache ujumbe huo juu ya maiti yake aende home akangojee waje. Awaulize, ninyi ni mahakama ya kuzimu au?? Kwani mnayesema nimemuua alikwisha kufa miaka 30 iliyopita. Mmemfufua au?
 
hahaaa duu.. kwa hiyo hapo unaaply sheria au mbinu za kisasi kijamii
 
hahaaa duu.. kwa hiyo hapo unaaply sheria au mbinu za kisasi kijamii

Hakuna kisasi wala sheria. Umeshalipia mali lazima uichukue. Mali zingine huharibika na hii ni mali delicate yaweza haribika.
 
Jamaa kaamua kutukumbusha enzi za amitha bachani! Nlikuwa nahudhuria pindi bila kukosa kwenye vibanda umiza! Hivi Ile move inaitwaje vile wahenge!
 
Nonsense...

Hakuna mahakama itafanya ujinga wa namna hii...

Waendesha mashtaki hutakiwa kuiaminisha na huthibitishia mahakama beyond any resoanable doubt kuwa ni kweli huyu mtu kaua.

Labda ndo maana unasema alifungwa "AKITUHUMIWA" ....ha ha haa..

Kiufupi ni kwamba hakuna mahakama itahukumu mtu bado akiwa "mtuhumiwa". Lazima atiwe hatiani kwanza mkuu.

Hivyo mpaka hapo kesi yako imekufa yenyewe yaani huyo mtu alikuwa hajafungwa maana hata kwenye record za makosa ya jinai za mahakama hatakuwemo. Maana alifungwa bila kutiwa hatiani kama criminal.
 
Alifungwa jela miaka 30 akituhumiwa kuua, lakini alipotoka gerezani akamuona aliyedaiwa kumuua, sasa kwa hasira akaamua kumuua, je sheria inasemaje au atahukumiwa tena kwa kuua?

Ni hayo tu kwa sasa.
Mahakama ya wapi hiyo?
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kuna movie yaitwa double jeopardy.

Mtu anatengeneza mpango kwamba ameuwawa na mkewe kwa lengo la kupata bima ya maisha.

Baadae mkewe anafungwa likini akiwa kwenye probation anagundua kwamba mumewe yupo na mama anamsaka huyo mume wake mfu, ili kumuua kwani akifanya hivyo anakuwa hana kosa.

Yaani huwezi kufungwa kwa kuua mtu huyuhuyo mara mbili.
 
Jamaa kaamua kutukumbusha enzi za amitha bachani! Nlikuwa nahudhuria pindi bila kukosa kwenye vibanda umiza! Hivi Ile move inaitwaje vile wahenge!
Andha kanoon
ok tuachane na movie,sasa vipi sheria inasema iwapo tukio kama hilo litatokea ?
 
Alifungwa jela miaka 30 akituhumiwa kuua, lakini alipotoka gerezani akamuona aliyedaiwa kumuua, sasa kwa hasira akaamua kumuua, je sheria inasemaje au atahukumiwa tena kwa kuua?

Ni hayo tu kwa sasa.
Kama hakumuua awali huyo ambaye inasemekana alimuua basi kimsingi na kisheria hakupaswa shitakiwa na kuhukumiwa kwa kosa la mauaji bali jaribio la kuua yaani 'attempt murder' na hilo tukio la pili baada ya kutoka jela ni mauaji ya kukusudia 'murder'.

Sheria itafuata mkondo wake na ile dhana ya mtu hawezi kuhukumiwa mara mbili kwa kosa lile lile, haiwezi simama wala kutumika kama defence hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…