Alihitaji namba Nikampa

Naisujaki Lekangai

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
1,340
Reaction score
1,377
Nimeshukia zangu barabara ya kibosho toka Arusha (wale wa kilimanjaro na Arusha wanalifahamu eneo) natafuta usafiri wa kwenda kindi kwa mama, namwona baba mmoja akinikimbilia."binti samahani" ananiambia huku akihema.Namsubiri na kumtazama usoni na nabaini nia yake."binti, naomba namba yako" Hasira zinanibana kwa kuitwa 'binti' lakini sizioneshi.

Anatoa simu yake aandike namba. Naanza, saba. kisha nanyamaza. "Inaanza na saba sio sifuri?"Anapayuka "Namba yangu ni saba"namsisitizia.Haandiki, anashangaa na kutezama huku na huko."Mtandao gani huo?"Sauti inamtoka.Namwelewesha kuwa hiyo ni namba ya saizi ya kiatu nachovaa si mtandao.

Mbaba anaguna na kuondoka akilalamika yeye alihitaji namba nikampa sasa shida nini?Wanaume bana!Mnapaparikia mtu kavaa pete ya ndoa?
 
Angekupa lift hadi kindi nadhani ungempatia tu namba ya simu
 
Unaongea kwa unyonge sana,

Inaonekana jamaa ulimpa namba na keshakutafuna,

Pole lakini kutafunwa ndo haki yenu ya msingi
 
Hujui kuna pete ya ndoa? By the way nilifunga ndoa 16 december 2017
Alichobugi ni kwamba hajajua kama mwenzake ndoa ndiyo unaianza utamu, mwaka mbele ukimuona utamkimbilia.

"We baba, we baba mi ndiyo yule binti nilikupa namba ya kiatu, leo nakupa namba ya chumba nitakachofikia"

Najua unajua kama natania
 
Wanawake wa Kindi wengi wenu mnakiwaga na matatizo ya aina hiyo, halafu wewe unajiona mjanja unakuja hadi kuchapisha mtandaoni.
 
Wanawake wa Kindi wengi wenu mnakuwaga na matatizo ya aina hiyo, halafu wewe unajiona mjanja unakuja hadi kuchapisha mtandaoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…