Naisujaki Lekangai
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 1,340
- 1,377
Nimeshukia zangu barabara ya kibosho toka Arusha (wale wa kilimanjaro na Arusha wanalifahamu eneo) natafuta usafiri wa kwenda kindi kwa mama, namwona baba mmoja akinikimbilia."binti samahani" ananiambia huku akihema.Namsubiri na kumtazama usoni na nabaini nia yake."binti, naomba namba yako" Hasira zinanibana kwa kuitwa 'binti' lakini sizioneshi.
Anatoa simu yake aandike namba. Naanza, saba. kisha nanyamaza. "Inaanza na saba sio sifuri?"Anapayuka "Namba yangu ni saba"namsisitizia.Haandiki, anashangaa na kutezama huku na huko."Mtandao gani huo?"Sauti inamtoka.Namwelewesha kuwa hiyo ni namba ya saizi ya kiatu nachovaa si mtandao.
Mbaba anaguna na kuondoka akilalamika yeye alihitaji namba nikampa sasa shida nini?Wanaume bana!Mnapaparikia mtu kavaa pete ya ndoa?