A
Anonymous
Guest
Kuna Kijana mmoja tulimtuhumu kumbaka Mwanangu wa miaka minne tukapeleka malalamiko kwenye vyombo husika vya Kiserikali, Jamhuri ikafungua kesi ya ubakaji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni.
Tumeenda Mahakamani mimi na Mke wangu kwa zaidi ya Mwaka mmoja na nusu, ambapo tulikuwa tukiacha shughuli za kutupatia kipato na kwenda Mahakamani ili tuone haki ya mtoto wetu kama itapatikana.
Mungu sio Athumani tukiwa tunaelekea kukata tamaa kutokana na shauri kusikilizwa kwa muda mrefu, hukumu ilitolewa jambo ambalo lilitupa faraja kutokana na gharama za nauli na muda mwingi tulivyokuwa tumetumia kwenda Mahakamani.
Hukumu iliyotolewa ni kwamba mtuhumiwa alitiwa hatiani kuhusika na kosa alilokuwa anatuhumiwa nalo. Hukumu hiyo kwetu ilileta nuru, faraja na kutufuta machozi tukiamini haki imetendeka baada ya awali kuhisi kuna mazingira ya danadana ambayo yalifanya haki kucheleweshwa.
Mshtakiwa baada ya kutiwa hatiani alihukumiwa kwenda jela miaka 30, ambapo hadi sasa ni takribani miezi mitano imepita.
Katika hali ya kusikitisha nuru imetoweka baada ya kuanza kumuona mtuhumiwa mtaani akiishi kama raia huru, ni kwa mara kadhaa tumemuona mtuhumiwa huyo huku jamaa zake wakifurahia kutoka gerezani.
Mimi sio mtaalamu zaidi wa Sheria lakini napata ugumu kuelewa kama Mtu aliyehukumiwa anaweza kurejea mtaani bila kushinda rufaa au kutolewa kwa kuzingatia taratibu nyingine za kisheria ikiwemo msamaha wa Rais.
Nimeshindwa kuweka taarifa zote kwakina ikiwemo namba ya kesi yenyewe na jina la mtuhumiwa ili kuepuka uwezekano wa walioshiriki mchezo huo kinyume kutopata fursa ya kumrejesha mtuhumiwa gerezani kupoteza ushahidi lakini nikihakikishiwa usalama na haki kutendeka naweza kutoa ushirikiano.
Kutokana na kile nilichokieleza naomba kama kuna wataalamu wanisadie kuelewa ni kwa namna gani mtuhumiwa anaweza kuwa uraiani tofauti na taratibu nilizoeleza, lakini vipi natamani kufahamu aina ya wafungwa ambao unufaika na msamaha wa Rais.
Kwa mwenendo huo napata mashaka kama watuhumiwa tunaoambiwa wamehukumiwa kama wapo ndani inavyotakiwa uenda wengine wapo nje tena kinyume na Sheria, KWAKWELI NIMEOGOPA!