Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,180
- 7,346
This is too much...
Hii inshu ilitokea miaka kadhaa iliyopita (miaka kama 18), maeneo ya Dodoma. Asubuhi na mapema dada mtu ambaye wakati huo alikuwa na miaka 3 na mtoto mmoja katika ndoa yake, alijiwa na mdogo wake wa kiume ambaye alikuwa amebeba mtoto mchanga. Waliongea pembeni kwa dakika ambazo hazikuzidi 10, then dada mtu akambeba yule mtoto akarudi nae ndani na mdogo mtu akaondoka. Mumewe yule dada akashangaa ile hali ikabidi amuulize mkewe, vipi mbona shemeji kaja gafla, mmeongea wenyewe na kakuachia mtoto, kuna nini. Hapo ndipo siri ilipoanzia... yule dada alikataa katakata kutoa details za yale mazungumzo au yule mtoto aliyeachiwa zaidi tu ya kusema mdogo wake amemuomba amlelee yule mtoto.
Mume alikomaa kutaka kujua ni nini kinaendeela lakini hakuambiwa kitu na mkewe wala shemeji yake (baba mtoto). Alijaribu kushirikisha wakwe ambao nao walipomhoji binti yao aligoma kueleza chochote. Inshu ilikuwa kubwa ikafika mahali mume mtu akamwambia mkewe, kama hasemi kitu arudi kwao, na yule dada akakubali bora arudi kwao kuliko aseme ile siri, tena akamuacha mwanae wa pekee aliyekuwa na miaka 2 tu kwa mumewe! Vikao vya familia upande wa mwanamke vilikaa na kuwashurutisha mtu na dada yake waeleze yanayomhusu yule mtoto, mama yake ni nani, lakini waligoma mwanzo mwisho, zaidi baba mtoto alipobanwa sana na maswali alikuwa analia...
Yule mtoto alikua na shangazi yake ambaye aliikacha ndoa yake, akimwacha mumewe kulazimika kuoa mwanamke mwingine miaka minne baadae. Alipofika darasa la tano, yule mtoto alianza tabia ya uma.laya, akawa gumzo mtaani, hata walipopiga, na kuadhibu kwa namna yoyote, kesi za kukutwa na waume za hazikupungua kila kukicha pale kwa bibi yake alipokuwa analelewa na shangazi na bibi (Bagamoyo). Tabia mbovu ya yule mtoto ilisababisha ahamishwe shule mara kwa mara, na mara ya mwisho alikuja kuishia Dar kwa ndugu lakini alitoroka shule akiwa la saba, akatoroka home, akaingia mtaani na hajulikani anaishi wapi, wala anafanya kazi gani, japo mara kwa mara anaonekana kwa baba wakubwa, au kwa bibi yake, hasa wakati wa matukio kama ya msiba, lakini hasemi anakaa wapi wala anakula nini mtoto wa kike mwenye miaka 18 sasa, na haya maisha ameyaanza tangia akiwa na miaka 13!
Cha kushangaza zaidi, hadi leo baba na shangazi yake yule mtoto hawajawahi kutoa details za yule mtoto...