Wakipekee
JF-Expert Member
- Aug 21, 2019
- 6,194
- 10,711
Acha kupotosha jamii..!Naona mada imewapita kushoto, kaongelewa AliKiba na ndie King of Bongo Fleva hata Mondi anajua hilo, mziki wa AliKiba unaishi milele kama vile leo tunavyosikiliza miziki ya kina Kenny Rodgers, Bob Marley, Michael Jackson, Phil Collins, Cliff Richard, Dolly Parton,n.k na tunaburudika utadhani tulikuwepo enzi zao, hao ndio Wanamuziki, wanasikilizika kwa rika lote na kizazi chote,
Mziki wa Mondi hauishi ni mchangamshaji ila hana nyimbo za kufanya zije zisikilizwe miaka 100 ijayo na kizazi kingine,
Natumaini umeelewa point yangu.
Tunakubali kweli alikiba ni msanii mzuri lakini isiwe tiketi ya kumponda diamond platinumz kua hana nyimbo zitakazoishi miaka mingi ijayo.... huu ni uongo na uzushi wa hali ya juu sana.
Nimeanza kumsikiliza alikiba tangu enzi zile za njiwa hata Nalia hadi leo hii mahaba.. ni msanii mkali aliyekamilika hasa kwenye angle tatu (uandishi mzuri, voko kali na melody bomba) lakini bahati nzuri pia hivo vitu vyote diamond anavyo na anakuja kumfunika alikiba kwenye kitu kimoja tu MAPINDUZI..(Tuachanae na hiyo angle)
Nirudi moja kwa moja kwenye hoja... Labda nikwambie tu Diamond ana ngoma kali zenye mistari mikali balaa labda kama we ni hater daraja la kwanza hivo hua husikilizi anachoimba Naseeb..
Hebu mfano niambie hizi ngoma nazoenda kutaja ipi ambayo ikipigwa mwaka 2040 itakua haina maana...
1. Kamwambie
2. Mbagala
3. Moyo wangu
4. Ukimwona
5. Mawazo
6. Nakukumbuka 1 & 2
7. Kesho
8. Lala salama
9. Number one
10. Nasema nawe
11. Wanaona gere
12. Nasema nawe
13. Utanipenda
14. Hunisumbui
15. Ntampata wapi
16. Eneka
17. Africa beauty
18. Hallellujah
19. Yatapita
20. Sikomi
Bila kusahau kolabo nyingi za kimataifa mfano Yope na Chacun pour soi aliyoimba na Papa Wemba...
Kwenye hizo ngoma hapo juu sijataja hata ngoma moja ya kubang.....
HEBU NIONESHE NGOMA AMBAYO HAITAPIGWA MIAKA HAMSINI IJAYO ISIKUPE HISIA