Alikiba: Sina bifu na Diamond lakini alinikosea na nikaumizwa na nilisha samehe

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Wasalaam!

Wana jamvi leo Msanii Alikiba ameamua kufungaka na kuweka waZi kili kinacho hitwa tofauti au bifu kati yake na Msanii Diamond!Kwanza lazima tukubaliane kuwa ALikiba ni mmoja wa Wasanii wasio penda maneno na malumbano na wasanii wenzie ndio maana hukaa kimya. Kwanza Alikiba alisema hana bifu na diamond na hana sababu ya kuwa na bifu nae japo yanayo ongelewa yana muumiza sana na aliamua kuondokana na hayo yote busara ya haraka ilikuwa kukaa kimya.

Aliendelea kusema aliumizwa sana aliposikia kuwa amefuta mistari ya diamond kwenye wimbo wa Single boy ambao aliimba na lady jaydee na hakuimba kabisa na diamond na hata producer aliye record wimbo huo alithibitisha. Aliendelea kusema kuwa aliumizwa sana na uongo huo kuhusu yeye na hakupenda kuuongelea sana kwa sababu ange onekana anatafuta kick wakati hakuKuwa na kitu kama hicho.

Pia Alikiba aliamua kusema kuwa aliumizwa sana na kitendo cha Diamond kufuta mistari yake kwenye wimbo wa Lala salama maana Diamond hakumwambia kwanini kafanya hivyo na hadi leo hakuwai kumwambia. Alisema hilo swala amechukulia kama na Kitendo cha mtu kuomba mtihani wako aangalizie alaf baadae ana kurudishia mtihani wako na kusema sitaki majibu yako au ana yafuta yote alaf unategemea atajisikiaje? na alisema yeye alisha samehe lakini Diamond alimkosea na hadi leo hawakuwai kukutana.

Ameweka wazi kuwa aliamua kuwa kimya ili watu waongee lakini hana tatizo na Diamond. Katika hili sikuona sababu ya Diamond kutomwambia Alikiba kuwa wimbo naufanya upya na nimetoa mistari yako maana sikuipenda na nimeamua kuimba mwenyewe.

Karibuni wana jamvi.
 
Ok safi

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Huwezi kuwa na bifu na mtu kienyeji hvyo, lazima kuna sababu
 
Ametumia busaraa saana Ally kiba, jamaa namkubali saana
 
Soon anaachia wimbo mpya..Duh kaamua arudi na Diamond watu wamuurumie wamwelewe.
 
Big up Ally K. Unabusara sana...nakukubal sanaaa
 
ona povu linavyokutoka,kiba n jesh la mtu mmoja.uwezo wake kimuzk n daimond mia moja.

Povu linamtoka Kiba wala sio mimi...Aliamua akae kimya kilichomuwasha aongee sasa ni nini kama sio kutafuta kick?? Anakaa kimya miaka,kurudi na singo mpya anaanza kumchokonoa diamond..Anataka kurudi kwa mgongo wa diamond uyo hana lolote.
 
Soon anaachia wimbo mpya..Duh kaamua arudi na Diamond watu wamuurumie wamwelewe.
Hakuna wala hatafuti kick! Kwa hiyo wewe unataka kusema ana Msingizia?
 
Naye akija kutoka kama diamond utamchukia tu wabongo mpo kama wachawi

kula gwara man!...uyasemayo ni kweli kabisa!....kitu ambacho wengi hawakijui ni kwamba ali kiba alivyokuwa juu alikuwa mjivuni sana hata hakuwa karibu na wasanii wenzake kama alivyo diamond leo!kiba is talented ila kwakuwa game ya bongo ni ya kupokezana kijiti (according to ruge mutahaba) huyu kiba hata afanye nini kufikia level alizokuwa awali ni ndoto za alinacha!his time has passed atabaki kukubalika kama ana kipaji ila hawezi kutoboa
 
Povu linamtoka Kiba wala sio mimi...Aliamua akae kimya kilichomuwasha aongee sasa ni nini kama sio kutafuta kick?? Anakaa kimya miaka,kurudi na singo mpya anaanza kumchokonoa diamond..Anataka kurudi kwa mgongo wa diamond uyo hana lolote.

hata ule mchiriku c mzur kivile,tuache hayo,ila turud kwenye kaul yako.Uwezo wa kiba c wa kuunganisha maneno ndio asikike,ili afike kwa kiba angekuwa bondia inabid apigane kwanza na rich mavoko,belly 9,unaona umbal huo then ndio ajipange kumpita kiba,wabongo n kama waingereza tu wakiamuau kukipamba kitu ukipamba kwel kwel.KIba n mkal,daimond n upepo tu umekubal
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…