Dah, the time wakati unaandika hii message was far away kwahiyo wala sikuona hiyo kitu! Kuhusu Mlela na PhD, ngoja Mlela nimuweke pending nimzungumzie Hemed.
Hemed namkubali sana kwenye movie kuliko muziki... na Hemed anaweza kuuza zaidi kwenye movie kuliko anavyoweza kuuza kwenye muziki...! Yule jamaa ni vile tu hajabahatika kupata script iliyoenda shule lakini ni bonge la muigizaji! Na hili la kutopata script zilizoenda shule wanasababisha zaidi wenyewe... wanadhani anyone can write a script na matokeo yake hawana best offer; na wala hawafahamu kwamba unaweza kwenda Kariakoo na kuchukua watu 100 at random na hapo ukapata waigizaji wazuri zaidi ya 50 lakini unaweza kufanya hivyo hivyo kwa upande wa script na usipate mwandishi mzuri hata mmoja! They're all not serious linapokuja suala la script! Kuna mtu aliwahi kunipa kazi yake; namuuliza muda wa kukamilisha kazi; akajibu anaihitaji within 2 weeks!!! Nikamjibu wazi kwamba am not that genius wa kuweza kumaliza script hata ndani ya mwezi mmoja achilia mbali hizo wiki mbili!